>>TFF YAKARIBISHA WADAU KUBUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA!
>>LIGI DARAJA LA PILI, SDL, KUANZA NOV 22!!
SOMA ZAIDI:
Release No. 171
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 5, 2014
NOOIJ AITA 24 STARS KUIKABILI SWAZILAND
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa
ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini
Mbabane.
Akizungumza
Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho
kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya
Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Gymkhana.
Novemba
11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla
ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji
walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na
Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar),
Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka
(Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua
(Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari
Kapombe (Azam).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba),
Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla
(Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji
ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo),
Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, DR Congo).
WADAU KUBUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni
mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na
ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
Mshindi
wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa
jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz
au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi
za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio
na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.
MPANDA UTD, UJENZI RUKWA KUANZA SDL
Michuano
ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 katika makundi
manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza
kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu ambapo Mpanda United itakuwa mwenyeji
wa Ujenzi Rukwa.
Mechi
hiyo ya kundi A itachezwa kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga.
Siku hiyo hiyo katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Mvuvumwa FC
na CDA (Lake Tanganyika, Kigoma), na Milambo dhidi ya Singida United
kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kundi
B mechi za ufunguzi ni kati ya Pamba na JKT Rwamkoma kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba huku Bulyanhulu FC ikiwa mwenyeji wa AFC kwenye Uwanja wa
Bulyanhulu mkoani Shinyanga.
Abajalo
FC ya Dar es Salaam itaikaribisha Kariakoo FC ya Lindi kwenye mechi ya
kundi C itakayochezwa Uwanja wa Karume. Nazo Kiluvya United na Transit
Camp zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani
Pwani.
Kundi
D mechi tatu za ufunguzi ni kati ya Town Small Boys na Volcano FC
(Uwanja wa Majimaji, Songea), Njombe Mji na Mkamba Rangers (Uwanja wa
Sabasaba, Njombe), na Wenda FC dhidi ya Magereza Iringa kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Nyumbani
»
» Unlabelled
» WACHEZAJI 24 WAITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KUJIANDAA KWA MECHI NA SWAZILAND NOVEMBER 16
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZILIZOSOMWA SANA
-
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupig...
-
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha mi...
-
Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzani...
-
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko...
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni