LOGO

http://www.michezoafrika.com/NewsImages/Shikanda_Azam.JPG
Aliyekuwa nahodha wa Azam FC Mkenya Ibrahim Shikanda ndiye aliyeteuliwa kuchukuwa nafasi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Azam FC Kally Ongala baada ya jumatatu ombi lake la kujiuzulu kukubalika kwa viongozi wa Azam FC. Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassoro, alilitabainisha kuwa, tayari wameshapata mrithi wa nafasi hiyo iliyoachwa na Kally. “Kuanzia sasa Ibrahim Shikanda ndiye atakayekuwa kocha wetu msaidizi mpaka hapo Kali atakapomaliza masomo yake japokuwa hatujui atamaliza lini,” alisema Nassor. Shikanda alikuwa akisimama mbadala wa Kally Ongala pale Kally alipokuwa akitingwa na shughuli nyingine kama vile michuano ya Kagame Cup, Shikand alikaimu nafasi ya Kally baada ya Kally kubaki nchini na baadhi ya wachezaji wa Azam FC waliokuwa wanacheza na Mtibwa Sygar katika mchezo wa usiku wa Matumaini.  Michuano hiyo ya Kagame ilifanyika nchini Rwanda mwaka huu, na Azam FC waliteuliwa kushiriki michuano hiyo baada ya Yanga kujitoa ikiwa imesalia siku chache kuanza kwa michuano hiyo.
Azam Fc iMEingia kambini leo jioni katika Hostel za Azam Complex, Chamazi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa siku ya Jumamosi, dhidi ya timu ya Coastal Union kutoka mkoa wa Tanga.
Beki Erasto Nyoni, aliyepata ajali juzi baada ya gari lake kugongana na mwendesha pikipiki, maarufu kama bodaboda anatarajiwa kuanza mazoezi jioni ya leo, baada ya kumaliza kesi yake Polisi.
Azam FC itaendelea kumkosa mshambuliaji Kipre Tchetche aliyekwenda nyumbani kwao, Ivory Coast kwa matatizo ya kifamilia, wakati beki Gardiel Michael ameanza mazoezi baada ya kukosa mechi dhidi ya Ndanda kwa kuwa majeruhi.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top