Timu ya soka ya Ureno leo usiku huu imefanikiwa kuichapa timu ya Argentina kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika dimba la Old Trafford nchini England
Bao hilo la pekee lilifungwa na Raphael Guerreiro katika dakika ya 90 ya mchezo. Mchezo huo ulikuwa kivutio kikubwa cha watu kwa kuwakutanisha wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa na wakiwa ni manahodha wa timu zao ambao ni Lionel Messi wa Argentina na Cristiano Ronaldo wa Ureno ambao wote walishindwa kucheka na nyavu hadi mwisho wa mchezo huo.
Hata hivyo kiungo wa Manchester United Angel Di Maria alipata majeraha kidogo mguuni na anatarajiwa kufanyiwa vipimo katika clinic ya Manchester United.
VIKOSI VILIKUWA NI
Argentina: Guzman
6, Roncaglia 5.5, Biglia 6, Demichelis 5.5, Ansaldi 6 (Silva 71, 5.5),
Mascherano 7, Otamendi 5.5, Pastore 6.5 (Pererya 73, 5), Di Maria 6
(Tevez 61, 5), Higuain 5.5 (Lamela 61, 5), Messi 7 (Gaitan 45, 6).
Portugal::
Beto 6.5, Bosingwa 6, Bruno Alves 6, Pepe 5.5 (Fonte 45, 6), Tiago
Gomes 5.5 (Guerreiro, 6); Nani 5, Moutinho 6, Danny 5.5 (Eder 45, 5.5),
Tiago 6 (Carvalho, 77) , Andre Gomes 5.5 (Silva 68, 5.5), Ronaldo 7
(Quaresma 45, 6)
Goals: Guerreiro 90,
Referee: Martin Atkinson (England) - 7.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni