BRAZIL MPYA YA DUNGA YAICHAPA AUSTRIA 2-1
Brazil, chini ya Meneja wao Dunga, wameendelea na wimbi lao la ushindi tangu ashike hatamu baada ya Usiku huu kuichapa Austria waliokuwa kwao Ernst Happel Stadium, Mjini Vienna Bao 2-1 katika Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki.
Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa Sare 0-0 ingawa Brazil walionekana kustahili kuwa mbele kwa kutawala na pia Refa wa Scotland, William Collum, kuwaminya Penati kadhaa.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 64, Brazil walifunga Bao kupitia David Luiz 64 aliefunga kwa Kichwa baada ya Kona lakini Austria walisawazisha kwa Penati ya Dragovic katika Dakika ya 75.
Penati hiyo ilitolewa kufuatia Oscar, Kiungo wa Chelsea, kumfyatua Weimann.
Hata hivyo, Mchezaji mpya wa Brazil, Roberto Firmino, anaechezea Klabu ya Germany 1899 Hoffenheim, aliipa ushindi Brazil kwa kigongo kikali cha Dakika ya 83.
Huu ni ushindi wa 6 mfululizo kwa Meneja Dunga tangu aitwae Brazil mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Julai.
VIKOSI:
Austria (Mfumo 4-2-3-1): Almer; Klein, Dragovic, Hinteregger, Fuchs; Kavlak, Ilsanker; Harnik, Junuzovic, Arnautovic; Okotie.
Brazil (Mfumo 4-2-3-1): Diego Alves; Danilo, Miranda, David Luiz, Filipe; Luis Gustavo, Fernandinho; Willian, Oscar, Neymar; Luiz Adriano
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni