LOGO

Ashanti United

Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara (FDL) inatarajiwa kuanza rasmi siku ya leo kwa timu 16 kushuka dimbani kusaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
Kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar, Friends Ranger watakuwa wageni wa Lipuli ya Iringa. Ashanti United watakuwa wageni wa Majimaji ya Ruvuma.
Mechi nyingine za kundi A zitashuhudia Kurugenzi ya Iringa ikiwaalika Tessema ya Dar wakati Kimondo ya Mbeya na Villa Squad kutoka Dar zikitoana jasho kwenye dimba la CCM Viwawa.
Kutakuwa na mechi nne kwenye kundi B. Maafande wa Polisi Tabora watapambana na Green Warriors kutoka Dar es Salaam kwenye uwanja wa Ali Hasssan Mwinyi.
Kikosi cha Panone ya Kilimanjaro kitaanza harakati zake za kupanda daraja kwa kupambana na JKT Kanembwa ya Kigoma kwenye uwanja wa Ushirika, Moshi.
Nao maafande wa JKT Oljoro watakuwa wenyeji wa maafande wenzao wa Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume.
Mechi nyingine ya kundi B itazikutanisha wenyeji Polisi Mara dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top