Na Boniface Wambura
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union
yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi
karibuni.
Uongozi wa Coastal Union
uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao tunautambua, na
tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.
Tunapenda kuwakumbusha
wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba
zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF
inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu.
Tayari tumepokea barua
kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia
kusimamishwa kwake.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni