Leo ni leo huko nchini ujerumani ambapo kuna mtanange wa kukata na shoka kati ya Mahasimu Bayern Munich na Borussia
Dortmund watakapovaana katika kugombea DFL Supercup mchezo utakao chezwa saa 1:00 usiku ndani ya dimba la Signal Iduna Park.
Kawaida Kombe hilo hugombewa na Bingwa wa Bundesliga na Mshindi wa
DFB-Pokal lakini Msimu uliopita vyote vilibebwa na Bayern na Dortmund,
maarufu kama BvB, kuambua Nafasi ya Pili katika ving’anyiro hivyo.
Hii itakuwa mara ya 15 kwa DFL Supercup kugombewa na ni mara ya 3 mfululizo kwa Bayern na Dortmund kukutana.
Mwaka 2012, Bayern walitwaa DFL Supercup kwa kuifunga Dortmund 2-1 na Mwaka Jana ilikuwa zamu ya Dortmund kuitwanga Bayern 4-2.
Safari hii mvuto mkubwa mbele ya Mashabiki 80,667 Uwanjani Signal Iduna Park ni kumwona Straika wa zamani wa Dortmund, Robert Lewandowski, akivaa Jezi ya Bayern kuikabili Dortmund kwa mara ya kwanza.
Lakini Kocha wa BVB Jurgen Klopp amesema Lewandowski atapokewa vizuri huko Signal Iduna Park na kusisitiza: “Ni mtu mwema na safi. Atapokewa vizuri tu lakini tuna nia kubwa na hii Supercup. Tunataka ushindi. Gemu na Bayern ni spesho. Wao ni moja ya Timu bora Duniani! ”
Pia, Timu hizi zitashusha Wachezaji zaidi ya 11 ambao walikuwepo kwenye Kikosi cha Germany kilichotwaa Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro Brazil hapo Julai 13 kwa kuifunga Argentina Bao 1-0 huku Bao lenyewe likifungwa na Mario Gotze, Mchezaji wa Bayern ambae kabla ya Msimu uliopita alikuwa akiichezea Dortmund.
Mshindi wa DFL Supercup safari hii ataweka Rekodi kwani kila Timu imeshatwaa Kombe hili mara 5 kila mmoja kwa Bayern kutinga Fainali 9 na kushinda 5 na Dortmund kuingia Fainali 7 na kushinda 5.
Hali za Wachezaji
Kila Timu itatinga ikiwakosa Masta wao kadhaa lakini BvB ndio wameathirika sana kwani watamkosa Marco Reus, kwa maumivu ya Enka, Nahodha wao Mats Hummels, tatizo la Musuli, Nuri Sahin na Jakub Blaszczykowski, wote Musuli, na Ilkay Gundogan, Mgongo.
Bayern wao watakuwa bila ya Rafinha, Enka, na Thiago Alcantara, Goti, na huenda wakamkosa Franck Ribery, mwenye maumivu ya Goti.
VIKOSI VINATARAJIWA:
BORUSSIA DORTMUND: Roman Weidenfeller, Lukasz Piszczek, Neven Subotic, Sokratis Papastathopoulos, Marcel Schmelzer, Sven Bender, Oliver Kirch, Pierre-Emerick Aubameyang, Milos Jojic, Henrikh Mkhitaryan, Ciro Immobile
BAYERN MUNICH: Manuel Neuer, Jerome Boateng, Javi Martinez, David Alaba, Pierre Hojbjerg, Philipp Lahm, Mario Gotze, Juan Bernat, Thomas Muller, Robert Lewandowski, Arjen Robben
Uso kwa Uso
Mechi za karibuni
17 Mei 2014 Borussia Dortmund 0 Bayern Munich 2 (German DFB Pokal)
12 Aprili 2014 Bayern Munich 0 Borussia Dortmund 3 (Bundesliga)
23 Nov 2013 Borussia Dortmund 0 Bayern Munich 3 (Bundesliga)
27 Julai 2013 Borussia Dortmund 4 Bayern Munich 2(German Super Cup)
25 Mei 2013 Borussia Dortmund 1 Bayern Munich 2 (UEFA Championz Ligi)
4 Mei 2013 Borussia Dortmund 1 Bayern Munich 1 (Bundesliga)
27 Feb 2013 Bayern Munich 1 Borussia Dortmund 0 (German DFB Pokal)

0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni