LOGO


Togo inahofia kucheza dhidi ya Guinea kufuatia mlipuko wa Ebola
Shirikisho la Soka barani Afrika imeagiza Guinea kuandaa mechi baina yake na Togo katika taifa mbadala kufuati mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola.
Agizo hilo linamaanisha mechi baina ya timu hizo mbili zilizopangiwa kuchezwa kati ya tarehe 5-6 Septemba hazitachezwa huko .
Aidha CAF imeagiza kuwa marufuku hiyo ya mechi nchini Guinea isalie hivyo hadi baada ya mwezi Septemba.
Togo iilikuwa meiomba shirikisho la soka barani Afrika CAF kuhamisha mechi baina yake na Guinea kuenda taifa mbadala ikihofia usalama wa wachezaji wake kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola.
Mechi hiyo iliyoratibiwa kuchezwa katia ya tarehe 5 na 6 Septemba ni ya kuwania kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika.
CAF yaagiza mechi hiyo isichezewe Guinea
Zaidi ya watu 300 wameaga dunia kufuatia mlipuko wa homa hiyo ya Ebola nchini Guinea huku wengine zaidi ya 700 wakiaga dunia Liberia na Sierra Leone.
''Ni jambo la kuogofya sana ''msemaji (TFF)
Shirikisho hilo TFF linauhakika kuwa serikali ya ya Togo huenda isiwaruhusu kwenda Guinea.
Mataifa mengi ya magharibi mwa afrika yamepiga marufuku mbali na kuweka mikakati dhabiti ya kuzuia kuenea kwa kwa homa ya ebola ambayo kufikia sasa imewaua zaidi ya watu 1000 .
BBC michezo imebaini kuwa Sierra Leone inapendekeza kucheza mechi hiyo nchini Ghana.
Msemaji wa shirikisho la Ghana Ibrahim Sane ameidhibitishia meza ya michezo ya BBC kuwa wamepokea ombi kutoka Sierra Leone na kuwa wanasubiri ruhusa kutoka kwa serikali na wizara ya afya .

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top