Argentina imemteua aliyekuwa
kocha wa Barcelona Gerardo Martino kuiongoza timu ya taifa baada ya
kung'atuka kwa kocha wa zamani Alejandro Sabella.
Martino, 51, alifurushwa kutoka Barca mwisho wa
msimu uliyopita baada ya kushindwa kushinda taji lolote kwa mara ya
kwanza tangu mwaka wa 2007.kocha wa zamani Sabella aliondoka baada ya kushindwa kwa bao moja kwa nunge na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Martino alimrithi kocha wa zamani wa Braca Tito Vilanova mwezi Julai 2013,Camp Nou baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka 2 .
Katika kipindi hicho Barca ilisajili ushindi katika mechi 40 kati ya 59 alizokuwa kocha lakini wakashindwa kusajili ushindi wowote wa tuzo la bara ulaya.
The Catalans walishindwa tena na vibonde wao Real Madrid katika fainali ya kuwania kombe la Copa del Rey.
Punde baada ya kuondoka kwake Camp Nou Barcelona,ilimteua Luis Enriqueas kurithi nafasi yake.
Atajulishwa rasmi hapo kesho (Alhamisi) kama mkufunzi wa Argentina.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni