LOGO

 yayaaa
Airtel Rising Stars kuzinduliwa Jumatano tarehe 17 Juni Dar es Salaam, Jumatatu 15 Juni 2015 . Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa huduma bora katika nchi 20 za Asia na Afrika, Bharti Airtel Afrika  imemtanagaza rasmi Yaya Toure kuwa balozi mpya kwa ajili ya kampeni mpya itakayozinduliwa hivi karibuni barani Afrika.
Ushirikiano huo kati ya Airtel na kapteni huyo wa Ivory Coast na kiungo wa Manchester City utaanza rasmi katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “It’s Now” yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia Nyanja mbalimbali kama vile michezo, ikijumuisha mashindano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ambayo mwaka huu yanatarajiwa Dar es Salaam, Jumatano, Juni 17.
Sehemu nyingine ambazo kampeni hii itazigusa ni kama vile mfumo mzima wa maisha na muziki, ambapo wateja watapata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kiteknolojia ili kuona fursa zinazowazunguka. Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Afrika, Christian de Faria amesema kuwa kampeni hii inadhihirisha nia ya dhati ya kampuni ya Airtel katika kuwaunga mkono vijana wa Afrika pia na kukuza fursa mbalimbali za kiuchumi.

Tunayo furaha kubwa sana kuingia mkataba na Toure, ambaye ana heshima kubwa sana Afrika na duniani kwa ujumla. Akiwa kama mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne mfululizo, Toure amekuwa ni kioo kwa vijana wengi ambao wanataka kufikia malengo yao,”de Fala amesema.
Akizungumzia ushirikiano wake na Airtel, Toure amesema, “katika kipindi chote ambacho nimetumika katika tasnia ya soka, nimekuwa ni
mwenye bahati kubwa sana kupata mkataba huu kutokana na mafanikio niliyoyapata uwanjani. Hata hivyo, najua kwamba unawezakucheza katika kiwango cha juu endapo utajitolea kwa asilimia 100 uwanjani.

“It’s Now” ni kampeni ambayo ipo moyoni mwangu kwani inalenga kuwaamsha vijana wa Afrika kuchangamkia fursa zinazowazunguka ili kuwa na maisha bora. Ninajivunia sana kufanya kazi na Airtel ambayo inafika maeneo mengi ya Afrika ili kuwapa ari vijana watu wengi.
Kwa upande wake, Colaso alisema, “Kwetu sisi hapa Tanzania kampeni hii ya It’s Now inaenda bega kwa bega na progamu ya Airtel Fursa ambayo ilizinduliwa mwezi Mei mwaka huu, pamoja na Airtel Rising Stars ambay inatarijia kuanza wiki hii. Tuna imani kubwa kuwa vijana wetu hapa nchini watakuwa na ari kubwa kutokana na uwepo wa Toure katika kampeni hii itakayojumuisha masuala ya michezo, maisha pamoja na muziki.
Tunawaasa vijana wenye nguvu na nia ya dhati kuikimbilia fursa hii ili kujikwamua wao wenyewe pamoja na familia zao.” Ushirikiano huu utampelekekea Toure kuunga mkono shughuli  za kijamii hasa kuwawezesha vijana kupata maendeleo. Ikiwa imeingia barani Afrika tangu mwaka 2010, Airtel Afrika imekuwa ikijiongezea wateja kufikia zaidi ya watu milioni 70.Kwa sasa Airtel ndio kampuni inayoongozwa kwa huduma bora za internet aina ya 3G katika nchi 17, huku pia ikitoa huduma z kifedha kwa njia ya simu za Airtel Money.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top