MIAMBA
ya kandanda ya Hispania, FC Barcelona imefanikiwa kutwaa kombe la tano
la Uefa Champions League baada ya kushinda 3-1 dhidi ya mabingwa wa
Italia, Juventus katika mechi ya fainali iliyopigwa usiku huu uwanja wa Olympic, mjini Berlin, Ujerumani.
Barcelona
walianza mchezo kwa kasi huku wakigongeana pasi za uhakika na katika
dakika ya tatu, Ivan Rakitic aliandika bao la kwanza akimalizia pasi
murua ya Andres Iniesta.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi
cha pili Juventus walijipanga na kusawazisha goli hilo kupitia kwa
Alvaro Morata aliyemalizia mpira uliotemwa na golikipa kutokana na shuti
kali la Carlos Tevez.
Dakika
ya 68' Lionel Messi alipiga shuti kali lililotemwa na kipa wa Juve,
Buffon na mpira kumkuta Luis Suarez aliyefunga goli ta pili na la
ushindi.
Dakika za nyongeza, Neymar akaifungia Barcelona goli la tatu kutokana na shambulizi la kushitukiza.
Barcelona chini ya Luis Enrique wamefanikiwa kutwaa makombe matatu msimu huu kwani awali walitwaa La Liga na kombe la Mfalme 'Copa del Rey'.
Hakika msimu wa 2014/2015 ulikuwa mgumu kwa walinzi wa timu za La Liga na Uefa Champions League kwasababu moto wa Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar Jr ni sawa na wa Petroli usiozimwa kwa maji.
TAKWIMU ZA MECHI YA LEO, BARCA KULIA, JUVENTUS KUSHOTO

VIKOSI
Juventus (4-4-2):
Buffon 8, Lichtsteiner 6, Barzaglia 7, Bonucci 7, Evra 6 (Coman 89);
Marchisio 7, Pirlo 6, Pogba 6, Vidal 6 (Pereyra 79); Tevez 6, Morata 8
(Llorente 85)
statistics :
Subs not used: Storari, Ogbonna, Llorente, Padoin, Sturaro.
Booked: Vidal, Pogba
Goal: Morata 55
Barcelona (4-3-3):
Ter Stegen 7; Alves 7, Pique 8, Mascherano 7, Alba 7; Rakitic 8
(Mathieu 90), Busquets 7, Iniesta 8 (Xavi 78); Messi 8.5, Suarez 8
(Pedro 90), Neymar 8 Subs not used: Bravo, Rafinha, Bartra, Adriano.
Booked: Suarez
Goals: Rakitic 4, Suarez 68, Neymar 90
Attendance: 70,442
Referee: Cuneyt Cakir (Turkey)
7
shots on target
8
8
shots off target
10
38
possession (%)
62
8
corners
6
1
offsides
0
24
fouls
12
2
yellow cards
1
14
goal kicks
9
1
treatments
1
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni