TIMU ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na
shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam
Jumanne saa 7 mchana.
Taifa Stars) jana usiku
imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON
mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 – 0 na wenyeji Misri.
Taifa Stars ilicheza vizuri
kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada
kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea
kwenda mapumziko -0 – 0.
Kipindi cha pili Misri
walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika
10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na Mohamed Salah (69).
Stars ilifanya mabadiliko ya
kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbdonde na kufanya
shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa
na walinzi wa timu ya Misri.
Mara baada ya mchezo huo, Taifa
Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na
shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam
jumanne saa 7 mchana.
Tanzania: Deogratias Munish,
Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub,
Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas
Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.
Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed
Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny,
Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa
Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni