CHAMA CHA MKOA DAR ES SALAAM DRFA KUHUSU KIPIGO CHA TAIFA STARS DHIDI YA MISRI 3-0 HAPO JANA
Na Omary Katanga, Dar
Chama cha kandanda mkoa wa Dar es Salaam DRFA, kimesikitishwa na matokeo mabaya iliyoyapata timu ya taifa (Taifa Stars) kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Mafarao wa Misri,katika mchezo wake wa kwanza uliopigwa jana usiku ugenini wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Mwenyekiti wachama hicho,Almas Kasongo, amesema matokeo hayo yamewafadhaisha mno watanzania wenye uchu wa kuona timu hiyo inapata matokeo mazuri yaliyokosekana kwa kipindi kirefu.
Amesema anaamini kuwa kikosi hicho kina wachezaji wazuri na wenye uwezo lakini wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya vizuri kwenye timu ya taifa hasa kwenye safu ya ushambuliaji, ikilinganishwa na uwezo wanaouonesha kwenye michuano ya ligi wakiwa na klabu zao.
Hata hivyo Kasongo amesema licha ya Stars kuanza vibaya katika harakati zake za kuwania tiketi yamichuano hiyo ya afrika,bado nafasi ipo ya kujipanga upya kwa kuanza kuangalia uwezo wa benchi la ufundi.
Aidha, amesema DRFA inaamini kuwa Tff inauwezo wa kutafuta mwarobaini wa kutibu tatizo la matokeo mabaya kwa Starz,bila kumuonea mtu aibu.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni