LOGO


 
 
 RATIBA
12:45 FC Porto ? - ? Basel
 
12:45 Real Madrid ? - ? Schalke 04

MECHI za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI zinaanza kuchezwa Jumanne Usiku Machi 10 kwa Mechi mbili.
Huko Santiago Bernabeu, Mabingwa Watetezi wa Ulaya, Real Madrid, wako kwao kurudiana na Schalke ya Germany ambayo waliitandika Bao 2-0 katika Mechi yao ya kwanzo huko Nchini Ujerumani.
Real wako kwenye nafasi murua kuwa Timu ya kwanza kutua Robo Fainali ya Mashindano haya kwani Mechi nyingine inayochezwa Jumanne Usiku ipo huko Ureno kati ya FC Porto na FC Basel ambazo zilitoka 1-1 katika Mechi yao ya kwanza huko Uswisi.
Jumatano Usiku, Machi 11, pia zipo Mechi 2 za Marudiano za Raundi hii kati ya Bayern Munich na FC Shakhtar Donetsk, zilizotoka 0-0 huko Ukraine, ambayo itachezwa Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany na nyingine ni ile itakayochezwa Stamford Bridge Jijini London kati ya Wenyeji Chelsea FC na Paris Saint-Germain ambazo zilitoka 1-1 huko Paris, France.
Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitakamilika Wiki ijayo kwa Mechi 4, mbili Jumanne Machi 17 na mbili Jumatano Machi 18.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top