
Endapo watafanikiwa kucheza timu ya
vijana ya klabu tajiri duniani, Real Madrid ya Uhispania, basi itakuwa ni
habari njema kwa soka la Tanzania, ambayo wachezaji wake kadhaa wamekuwa
wakifeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa ughaibuni, hasa nchi za Ulaya katika
miaka ya nyuma.
Kufuatia tetesi za kutakiwa kwenda
kufanya majaribio Real Madrid, mashabiki wa soka wa klabu ya Simba ya Dar es
Salaam wamewaombea wachezaji wao kila la kheri katika majaribio yao ili waweze
kusakata kabumbu Ulaya.
Haruna Hamisi, mmoja wa mashabiki na
mwanachama wa Simba amesema beki wa kati wa klabu hiyo, Hassan Isihaka na
straika Ramadhan Singano anayejulikana kama "Messi" kwa jina la
uwanjani wana uwezo wa kucheza soka la kulipwa.
‘Vipaji tunavyo, ila vinakosa nafasi
na kuharibiwa na mfumo wetu mbaya wa kutolea wachezaji wakiwa bado wadogo”,
alisema Hamisi.
Emmanuel Temaeli, shabiki mwingine
amesema endapo watafanikiwa, basi itakuwa faida si tu kwa Simba, bali taifa
zima.
“Tukiwa na wachezaji wengi
wanaocheza soka nje, tutakuwa na timu ya taifa imara kwa ajili ya michuano
mbalimbali kama vile ya Mataifa ya Afrika na michuano ya kufuzu kucheza kombe
la dunia”, alisema Temaeli.
Taarifa zinasema kuwa klabu ya Real
Madrid ya Hispania, ambayo maofisa wake wamekuja nchini kuingia ubia na shirika
la hifadhi ya jamii (NSSF) kujenga kijiji cha michezo kwa ajili ya kulea
wachezaji vijana kitakachosimamiwa na klabu hiyo ya Cristiano Ronaldo, wameomba
CD (video) ili wawafanyie tathmini kupitia mechi walizocheza hivi karibuni.
Mabosi hao wamevutiwa na wachezaji
hao vijana baada ya kuwaona katika mechi ya ligi kuu wakati Simba ilipocheza na
klabu tajiri ya Azam na kutoka sare ya 1-1 majuma mawili yaliyopita.
Wachezaji kadha wa Tanzania
wamefanikiwa kufanya majaribio kucheza nje bila mafanikio akiwemo mshambuliaji
machachari, Mrisho Ngasa (anayecheza Yanga hivi sasa) aliyekwenda kufanya
majaribio klabu ya West Ham ya Uingereza mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha
Gianfranco Zola.
Hivi karibuni, CSKA ya Urusi
imemchukua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na mchezaji
wa klabu tajiri barani Afrika ya TP Mazembe ya Congo (DRC), Mbwana Samatta kwa
ajili ya majaribio na tetesi zinasema mabosi wa timu wamevutiwa naye licha ya
kuendelea kumjaribu
bbc swahili
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni