
Hiyo Jumamosi, kwenye Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi huko White Hart Lane, Wenyeji Tottenham wataikaribisha Arsenal kwenye Dabi ya London ya Kaskazini na Mechi hii licha ya kuwa ni Dabi pia ina ushindani wake wa kulilia kuwemo 4 Bora kwani Arsenal wako Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 mbele ya Tottenham walio Nafasi ya 6.
Mechi ya mwisho kwa Siku ya Jumamosi ni ile Dabi ya Merseyside Jijini Liverpool Uwanjani Goodison Park ambako Everton wataikaribisha Liverpool.
Katikati ya Dabi hizo mbili zipo Mechi 5 za Ligi zikiwemo ile ya Vinara wa Ligi Chelsea wakiwa Ugenini huko Villa Park kucheza na Aston Villa na Mabingwa Watetezi Man City kuwa Nyumbani Etihad kucheza na Hull City.
Jumapili zipo Mechi 3 za Ligi na mojawapo ni ile ya Uwanjani Upton Park wakati West Ham watakapoikaribisha Man United ambao wako Nafasi ya 3 kwenye Ligi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Saa za Bongo
Jumamosi Februari 7
1545 Tottenham v Arsenal
1800 Aston Villa v Chelsea
1800 Leicester v Crystal Palace
1800 Man City v Hull
1800 QPR v Southampton
1800 Swansea v Sunderland
2030 Everton v Liverpool
Jumapili Februari 8
1500 Burnley v West Brom
1705 Newcastle v Stoke
1915 West Ham v Man United
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni