LOGO

MASHINDANO ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, yameendelea Leo baada ya Jana kuchezwa Mechi mbili za ufunguzi za Kundi A na Leo Zambia kutoka Sare 1-1 na Congo DR katIka Mechi ya kwanza ya Kundi B iliyochezwa Nuevo Estadio de EbebiyĆ­n Mjini Ebibiyin.
Zambia walitangulia kufunga katika Dakika ya Pili tu wakati Given Singuluma kumzidi Kipa wa Congo DR, Kidiamba, ambae wote huchezea Klabu ya TP Mazembe huko Lumbumbashi.
Lakini Congo DR wakasawazisha kwa Bao la Dakika ya 66 Yannick Bolasie anaechezea Klabu ya Ligi Kuu England, Crystal Palace.
Baadae Leo itachezwa Mechi ya Pili ya Kundi B kati ya Tunisia na Cape Verde.
VIKOSI:
DR Congo: Muteba, Djos, Kilichio, Mbemba, Mongongu, Mpela, Kage, Mulumbu, Bolasie, Ndombe, Mbokani
Akiba: Oualembo, Omba, Makiadi, Kebano, Bawaka, Kalonji, Zakuani, Kudimbana, Mabwati, Bokila, Mabidi, Mandanda.
Zambia: Mweene, Mbola, Sunzu, Nkausu, Lungu, Sinkala, Kalaba, Singulama, Mayuka, Kampamba
Akiba: Munyao, Munthali, Kabwe, Sautu, Musakanya, Mukuka, Musonda, Kangwa, Mwanza, Titima, Ngoma
REFA: Ghead Grisha [Egypt]

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top