Mabao matatu (Hat-Trick) yaliyofungwa na
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na bao la jioni kutoka kwa
Kpah Sherman yalitosha kuwapatia ushindi mnono watoto wa Jangwani timu
ya Yanga kwenye mchezo wao wa kwanza kwenye kombe la Mapinduzi
walipovaana na timu ya Taifa ya Jang'ombe.
Mchezo huo ulishuhudia Yanga wakitawala
kwa kiasi kkubwa kwenye kila idara na hasa katika kumilika mpira
kutokana na kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm kuwaanzisha wachezaji
wenye kasi.
Hans alianza na Mrisho Ngassa, Andrey
Coutinho, Simon Msuva, Hassan Dilunga na Salum Telela kwenye kiungo kitu
kilichowawia vigumu vijana wa Jang'ombe kutawala mchezo huo.
Pamoja na mabao hayo ya Yanga, bado safu
ya ulinzi hasa mabeki wa kati walionekana kufanya makosa mara kadhaa
ambapo Nahodha Nadir Haroub alicheza na Pato Ngonyani na kama
washambuliaji wa Jang'ombe wangekuwa makini, wangeweza kujipatia mabao
hasa kipindi cha kwanza.
Matokeo hayo yanakamilisha idadi ya timu
nne zinazoshiriki michuano hiyo kutoka Tanzania bara kukamilisha
mzunguko wa kwanza wa makundi hayo huku Simba ikiwa ndiyo timu pekee
ambayo haina alama hata moja baada ya hapo jana kufungwa bao 1-0 na
Mtibwa Sugar huku Azam Fc kwenye mchezo wa mapema leo wakitoka sare ya
bao 2-2 na KCCA ya Uganda.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZILIZOSOMWA SANA
-
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupig...
-
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha mi...
-
Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzani...
-
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko...
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni