
Man City wao wako Nafasi ya Pili Pointi 2 nyuma ya Vinara Chelsea na Arsenal wako Nafasi ya 5 Pointi 1 nyuma ya Man United.
City wataingia kwenye Mechi hii bila ya nguzo yao muhimu, Yaya Toure, ambae hivi sasa yuko huko Equatorial Guinea akiwa na Timu ya Taifa ya Ivory Coast ambayo inashiriki AFCON 2015, Kombe la Mataifa ya Afrika, linaloanza Leo hii.
Pamoja na Toure, pia kwenye Timu hiyo ya Ivory Coast yupo Mchezaji mpya wa City, Wilfried Bony, waliemnunua Juzi kutoka Swansea City.
Licha ya upungufu huo, Meneja wa City, Manuel Pellegrini, amesema wanacho Kikosi imara kuziba pengo lolote.
Kila Timu ina tegemezi lake huku City wakimtegemea sana Sergio Agüero, ambae sasa amerejea tena baada ya kupona maumivu na Arsenal hivi sasa kila kitu ni Alexis Sánchez.
Lakini pia kila Timu itawakosa Majeruhi kadhaa kwa City kuwakosa Samir Nasri na Edin Dzeko huku Arsenal wakiwa na mlolongo wa kina Kieron Gibbs, Welbeck, Wilshere, Arteta, Debuchy, Diaby na Gnabry.
Msimu huu, Man City na Arsenal zimeshakutana mara mbili kwa Arsenal kushinda Mechi ya kwanza ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Hisani na kisha kukutana kwenye Ligi na kutoka Sare 2-2 Uwanjani Emirates.
Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii, Arsenal walibamizwa Bao 6-3 na kwa Miaka Mitano iliyopita hawajaambua ushindi wakicheza Ugenini Jijini Manchester.
MSIMU ULIOPITA MECHI KAMA HII:
Man City 6 Arsenal 3
Hata hivyo, safari hii Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesisitiza kuwa ni muhimu Kikoso chake kuwa na uwiano mzuri kutoka Difensi, Kiungo na Ushambuliaji wao lakini Wachambuzi wamedai ili kupata hilo ni muhimu Kikosi chake kiwe na Kiungo Mkabaji mzuri na ukimwondoa Flamini, Arsenal wanapwaya mno kwenye Idara hiyo.
Lakini hii ni Mechi muhimu kwa kila Timu kwa Arsenal kuwania kuingia 4 Bora na Man City wakiifukuza Chelsea kileleni hasa baada ya Mechi hii inabidi City wasafiri kwenda Stamford Bridge kucheza na Chelsea hapo Januari 31.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN CITY: Hart, Zabaleta, Demichellis, Kompany, Kolarov, Fernandinho, Fernando, Navas, Silva, Milner, Aguero
Akiba: Caballero, Wright, Sinclair, Sagna, Boyata, Lampard, Clichy, Pozo, Dzeko, Jovetic, Mangala
ARSENAL: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquellin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Sanchez, Giroud
Akiba: Martínez, Szczesny, Özil, Chambers, Hayden, Flamini, Rosicky, Campbell, Walcott, Akpom, Gibbs
REFA: Mike Dean
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni