LOGO

MASHINDANO ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, yanaanza Leo Jumamosi Januari 17 na Nchi 16, wakiwemo Wenyeji Equatorial Guinea, watachuana kwa kuanzia Mechi za Makundi.
Yapo Makundi Manne ya Timu 4 kila mmoja na Timu mbiliza juu toka kila Kundi zitaingia Robo Fainali.
Mechi za Makundi zitachezwa katika Miji ya Bata, Malabo, Mongomo na Ebebitin.

VIWANJA:
-Estadio de Bata, Mjini Bata, Watazamaji 37,500
-Nuevo Estadio de Malabo, Malabo, Watazamaji 15,250
-Estadio de Mongomo, Mongomo, Watazamaji 10,000
-Nuevo Estadio de EbebiyĆ­n, Ebebitin, Watazamaji 5,000

Leo zipo Mechi mbili za ufunguzi za Kundi A na ya kwanza ni ya Wenyeji Equatorial Guinea watakapocheza na Congo ndani ya Estadio de Bata Mjini Bata na kufuatia Mechi ya Burkina Faso na Gabon Uwanjani hapo hapo.
Kila Siku kutakuwa na Mechi mbili na Fainali ya Mashindano haya itachezwa Februari 8, Estadio de Bata, Mjini Bata.
Awali Mashindano haya yalikuwa yachezwe Nchini Morocco lakini Nchi hiyo ilijitoa kwa kuhofia Ugonjwa wa Ebola uliolipuka huko Afrika Magharibi na CAF kuipa Uenyeji Equatorial Guinea Nchi ambayo Mwaka 2012 iliweza pia kuwa Mwenyeji wa Mashindano haya pamoja na Gabon ambapo Zambia waliibuka Mabingwa.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top