Timu ngumu na inayoongoza ligi kuu nchini England Chelsea leo siku ya mwaka mpya wameweza kukutana na dhahama ya magoli 5-3 kutoka kwa Tottenham hotspurs katika mchezo wa mwisho wa siku ya leo ya mwaka mpya katika dimba la White heart line.
Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupita kwa Diego Costa baada ya kazi nzuri kufanya na Eden Hazard katika dakika ya 18 ya mchezo huo uliokuwa mkali na wakusisimua, bao lilidumu hadi dakika ya 30 baada ya Keane kusawazisha goli hilo na kufanya ubao kusomeka 1-1 katika dakika ya 44 Rose aliipatia Spurs goli la pili huku kila mtu akiamini kuwa mapumziko timu zitakuwa 2-1 Townsend aliipatia Spurs goli la 3 baada ya Keane kuangushwa eneo la hatari na kufanya Kocha wa Chelsea kuondoka uwanjani na kukimbilia vyumbani kabla ya filimbi ya mapumziko kupigwa.
Spurs inayofundishwa na Mauricio Pochettino iiendeleza moto katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata goli la 4 lililofungwa na Harry Keane katika dakika ya 52 likiwa ni bao lake la pili katika mchezo huo, Chelsea walijitahidi kupunguza idadi hiyo ya magoli kwa kujipatia bao la pili kupitia kwa Eden Hazard katika dakika ya 61 ya mchezo huo.
Wakati Chelsea wakitafuta namna ya kurudisha magoli hayo Necer Chadli alishindilia goli la 5 kwa Chelsea na kukata matumaini ya Chelsea kurudisha goli hizo, lakini katika dakika ya 87 John Terry aliifungia Chelsea goli la 3 mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho Spurs wameibuka na ushindi wa goli 5-3 na kuwapa faida Man City kwa kuwafikia pointi Chelsea
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Fazio, Vertonghen, Rose (Davies - 76'), Bentaleb, Mason (Dembélé - 14'), Chadli, Eriksen, Townsend (Paulinho - 66'), Kane
Akiba: Vorm, Chiriches, Davies, Dembele, Paulinho, Stambouli, Soldado.
Chelsea: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Willian (Salah - 72'), Oscar (Ramires - 45'), Hazard; Diego Costa
Akiba: Cech, Zouma, Mikel, Ramires, Salah, Remy, Drogba.
REFA: Phil Dowd
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni