LOGO

 
Simba SC leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza katika ligi kuu ya vodacom msimu huu, baada ya kucheza michezo 7 bila kupoteza wakitoa sare michezo 6 na kushinda mchezo mmoja.
Simba sc hii leo wamefungwa katika uwanja wa taifa na kagera sugar mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo simba sc walitawala mchezo mzima huku wakishindwa kupenya katika ngome ya kagera sugar na nafasi chache walizo zipata kupitia kwa Danny Sernkuma walishindwa kuzitumia, wakati kagera sugar wakitawala kwa muda mchache kwa nyakati tofauti nakufanikiwa kutengeneza nafasi mbili.

Nafasi ya kwanza ya kagera sugar yalitokana na makosa ya kipa Ivo Mapunda katika dakika ya 22 ya mchezo ambapo Ivo alitoka golini kujaribu kudaka mpira uliorushwa, ambao ulimshinda na mpira ukamkuta Atupele Green ambaye aliiandikia goli la kuongoza kagera sugar.

Nafasi ya pili ilikuwa katika dakika ya 80 wakati simba sc walipo enda kushambulia na nahodha wa kagera kufanikiwa kuupoka mpira na kusogea nao kabla ya kumpasia Atupile na kupiga krosi iliyomkuta Nongwa na kuunga krosi hiyo, huku Ivo akisimama imara kuucheza mpira huo.

Mara kadhaa simba sc walijaribu kupiga mashuti ambayo yaliishia mikononi mwa kipa ama kutoka nnje ya lango na huku krosi za Hassan Kesi zikiishia kwa kipa ama mabeki kuucheza.

Kuna krosi aliyopiga Kessy na kutua kichwani kwa Maguli, ama nusura izae goli lakini kipa wa kagera sugar aliuwahi na kuupangua na kuzaa kona isiyokuwa na mazara.

Mpaka kipenga cha mwisho kinapuliza kagera sugar 1-0 simba sc. Na kagera sugar wakifikisha pointi 13 kama yanga na azam fc.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top