Wiki endi hii siku ya jumapili dunia itashuhudia mtanange
mkali wa kukata na shoka kutoka kwa timu zinazoaminika kuwa na ushindani au
upinzani mkubwa nchini England kutokana na historia zao mchezo huo utachezwa
majira saa 10:30 kwa saa za Kitanzania..
Timu hizi zinapokutana shuhuli nyingine husimama kupisha
mtanange huu mkubwa duniani ambao umeshasababisha vifo vya Mashabiki wengi tu
wa Clabu hizi Maarufu duniani na Nchini England.
Manchester United inayofundishwa na Mdachi Louis van Gaal
inaikaribisha Liverpoolinayofundishwa na Brendan Rodgers huku ikiwa na muenendo
mzuri kwenye ligi ambapo wameshinda mechi 5 mfululizo huku Liverpool ikiwa na
muenendo usioridhisha baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Sunderland
katika mchezo wa ligi ulioisha.
Mancheseter United ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi
kuu nchini England EPL mara baada ya kuifunga Southampton huku vijogoo wa
Liverpool wakiwa nafasi ya 9 huku katikati ya wiki hii wakiondoshwa nje ya
michuano ya Uefa Champions League na timu ya FC Basel ya Uswisi.
Katika mchezo wa mwisho wa timu hizi kukutana kule nchini
Marekani katika mechi za Pre Season Manchester United ilishinda jumla ya magoli
3 kwa 1 lakini mara yamwisho kukutana kwenye Ligi kuu Manchester United
iliambulia kipigo kikali kutoka kwa Liverpool cha jumla ya Magoli 3-0 huku Man
united ikiwa chini ya David Moyes mchezo huo ulifanyika kwenye dimba la Old
Traford ambapo mwamuz Mark Clatenburg aliechezesha mchezo huo aliwazawadia
Liverpool penalt 3 huku Nahodha Steven Gerrard akifunga mbili na Luis Suarez
akifunga goli 1.
Kuelekea Mchezo huo Manchester United inaingia dimbani ikiwa
na Majeruhi kibao ambapo Angel Di Maria bado atakosekana kweye mchezo huo
kutokana na tatizo la Hamstring huku Chris Smalling akikiosekana pia baada ya
kuumia kwenye mchezo ulipita huku Liverpool ikiendelea kumkosa Mshambuliaji
wake Mahiri Daniel Sturidge na Rickie Lambart huku beki Kolo Toure akirejea
dimbani ambapo alicheza mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya FC Basel.
Timu hizo ambazo bado zinamatatizo ya Defensi zitaingia
uwanjani huku zitigemea mbinu za makoxha zaidi katika kuamua mshindi wa mchezo
huo au uwezo binafsi wa wachezaji wao nyota kama Robin van Persie, Wayne
Rooney, Raheem Sterling na Felipe Coutinho.
Kocha Manchester United amewaonya wachezaji maarufu wa
zamani timu hiyo kuwaache kuiongelea vibaya timu hiyo kwani hawajui
kinachoendelea klabuni hapo hiyo imetokana Garry Nevile na Paul Scholes kuanza
kuiongelea vibaya timu hiyo na kusema inacheza kama bata au mbwa haieleweki.
MCHI 5 ZA MWISHO KUKUTANA
·
United 0-3 L'pool (PL, Mar 14)
·
United 1-0 L'pool (LC, Sep 25)
·
L'pool 1-0 United (PL, Sep 13)
·
United 2-1 L'pool (PL, Jan 13)
·
L'pool 1-2 United (PL, Sep 12)
TIMU ZILIVYOKUTANA
MANCHESTER UNITED IMESHINDA 75
LIVERPOOL IMESHINDA MARA 64
SARE NI MECHI 51
TAKWIMU ZA WACHEZAJI
Steven Gerrard ndio mchezaji
aliefunga magoli mechi Old Trafford magoli 5
Robin van Persie amefunga magoli 6
katika mechi 9 za mwisho dhidi ya Liverpool
Juan Mata amefunga magoli 4 katika
Mashuti 5 yaliyolenga goli shots on target
|
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni