Kikosi
cha timu ya Young Africans tayari kimesharejea jijini Dar es salaam
kutok kanda ya Ziwa ambapo kilicheza michezo miwili ya Ligi Kuu ya
Vodacom dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga na Kagera Sugar ya
mjini Bukoba na kujikusanyia pointi tatu kati ya pointi sita.
Mara
baada ya kurejea jijini Dar es salaam kocha Marcio Maximo alitoa
mapumziko ya siku moja kwa wachezaji wake kabla ya leo jioni kuanza
mazoezi ya Gym eneo la Posta kuweka mili safi lna kesho kuendelea na
mazoezi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola
Akizungumzia
mechi mbili zilizochezwa kanda yta ziwa, Maximo amesema walijitahid
kucheza na kusaka ushindi kwa nguvu zote lakini pia timu walizocheza
nazo zilikua nyumbani na kupambana kuhakikisha nazo hateztipotezi mchezo
nyumbani.
"Tumepata
pointi tatu kati ya sita katika michezo miwili ya ugenini kanda ya
ziwa, mechi zilikuwa ngumu wenyeji waliicheza kwa nguvu kusaka pointi
viwanja vya nyumbani hali iliyotupelekea kupata ushindi wa mchezo mmoja
na kupoteza mchezo mmoja"alisema Maximo
Aidha
Maximo amesema mchezo dhidi ya Kagera Sugar mwamuzi alishindwa kulimudu
pambano, mechi haikuchezwa kwa dakika 90 kutoka na kusimama kwa zaidi
ya dakika 10 kutokana na wachezaji wa Kagera kupoteza muda, lakini
katika hali ya kustajabisha waliongeza dakika tatu tu ambazo pia
mchezaji wa wakata miwa alitumia kutibiwa ndani ya Uwanja.
Kiukweli
kuna wakati mgumu sana kwa soka la Tanzania kufika hatua za juu,
waamuzi wamekua na makosa mengi ambayo yanaonekana dhahiri, lakini pia
Uwanja wa Kaitaba haufai kwa kuchezewa kwa Ligi kuu kwani mbovu kupita
kiasi, kwani pia unatumka kwa shuguli za mashindano ya Pikipiki na
maonyesho mbalimbali.
Young
Africans inatarajia kucheza na Mgambo JKT siku ya jumamosi kwenye dimba
la Uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam mchezo ambao kocha Maximo
amesema ni muhimu kupata pointi tatu ili kurejea katika nafasi mbili za
juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni