MUDA
wowote wiki hii Simba inaweza kumalizana na straika namba moja wa
Elverum FC ya Norway, Minigeria Emeh Izuchukwu. Mchezaji huyo akiwa na
mwenzake, Orji Obinna, waliwahi kutamba na Simba mwaka 2008 wakitokea
Enyimba ya kwao Nigeria.
Wachezaji
hao waliondoka nchini kwenda kusaka noti Ulaya, lakini sasa Emeh
amefanya mazungumzo ya kina na Simba na wakati wowote wiki hii anaweza
kumalizana nao na kutua nchini, Mwanaspoti limethibitishiwa.
Mbali
ya hao, pia Simba imewapandisha ndege wachezaji watatu kutoka jijini
Mbeya kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo na kuwasainisha mikataba.
Wachezaji hao ni beki wa kati Nurdin Chona na beki wa kulia Salum
Kimenya wote kutoka Prisons ambao walitua jijini Dar es Salaam Jumamosi
wakati mshambuliaji wa Mbeya City, Deus Kaseke, aliingia jana Jumatatu.
Taarifa
za kuaminika ambazo Mwanaspoti ilizipata jana Jumatatu ni kwamba vigogo
wa Simba walikutana na mchezaji mmoja mmoja kwa nyakati tofauti ambapo
ilielezwa kwamba Chona ametaka dau la Sh 30 milioni, Kimenya ameanzia
Sh25 milioni huku Kaseke akitaka kupewa Sh40 milioni, hata hivyo vigogo
hao wamesema kwamba kwao fedha sio tatizo.
Wachezaji
hao ni mapendekezo ya viongozi baada ya kocha wao Patrick Phiri kutoa
baraka kwa viongozi kumsaidia kusaka wachezaji wazuri kwa maelezo kwamba
bado hawajui vizuri wachezaji wote wenye viwango vya juu vya kuichezea
Simba huku wakipendekeza pia jina la Said Morad wa Azam FC.
Phiri
yeye katika ripoti yake aliyoikabidhi alipendekeza majina ya wachezaji
wa Mtibwa Sugar mshambuliaji Ame Ally na beki Hassan Kessy, Danny
Mrwanda (Polisi Moro) na Dan Sserunkuma wa Gor Mahia ya Kenya ambaye
tayari wameshaanza mazungumzo. Hata hivyo uwezekano wa kumpata Mrwanda
ni mdogo kwani anarudi Vietnam alikokuwa akicheza soka la kulipwa.
Phiri
alitaka pia atafutiwe wachezaji wa nafasi mbalimbali ikiwemo beki ya
kulia na kushoto, beki ya kati, kiungo, straika na kipa ambapo imedaiwa
kuwa Juma Kaseja atarejea Simba wakati wowote kwani tayari amevunja
mkataba wake na Yanga.
Kwa
upande wa viongozi wa Simba walisema wamezungumza na wachezaji wengi
hasa nafasi ya straika na beki na wanaamini watafanikiwa kwa asilimia
kubwa.
Simba
ndiyo timu pekee inayoonekana kuhaha kwenye usajili wa dirisha dogo
kuhakikisha inapata wachezaji wazuri kutokana na matokeo yao
waliyoyapata katika mechi saba za kwanza za Ligi Kuu Bara msimu huu
ambapo ilitoka sare mechi sita na kushinda mechi moja tu. Ipo katika
mpango wa kuwatema wachezaji wake kadhaa akiwemo Uhuru Seleman, Ivo
Mapunda, Amri Kiemba ambaye Azam wanamhitaji.
Wengine
ni Mrundi Pierre Kwizera anayedaiwa kupelekwa kwa mkopo Afrika Kusini
pamoja na Joram Mgeveke anayetafutiwa timu ya mkopo, Nassoro Masoud
‘Chollo’ na Haruna Chanongo ambao wanatajwa kuachwa kutokana na madai ya
kushuka kwa viwango vyao.
Mwanaspoti
Mwanaspoti
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni