MATAJIRI
Azam FC wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumnasa straika Mmali wa El
Merreikh, Mohamed Traore ambaye anatarajiwa kutua nchini mwishoni mwa
mwezi huu kwa mazungumzo ya mwisho, pia klabu hiyo imetangaza dau
analouzwa Muivory Coast wao, Kipre Tchetche ni Sh336 milioni.
Traore
atawasili nchini baada ya kumaliza mechi yake ya Jumatano ijayo ambayo
atakuwa akiichezea timu yake ya Taifa ya Mali itakayocheza na Algeria
kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na atakuwa
mchezaji wa pili kutoka El Merreikh baada ya Muivory Coast Pascal Wawa
aliyepewa mkataba wa miaka miwili.
Azam
inamsajili Traore ambaye atakuwa mchezaji wa tano wa kigeni baada ya
Tchetche, Wawa, Muivory Coast Kipre Bolou, Mrundi Didier Kavumbagu na
Mhaiti Leonel Saint-Preux baada ya kumtupia virago Mmali, Ismail Diara.
Na
ili kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni wanaohitajika Ligi
Kuu Bara, inaweza kumuuza Tchetche ambaye anatakiwa na klabu mbalimbali
kutoka Malaysia na Sri- Lanka kwa makubaliano ya kulipwa kiasi hicho cha
pesa au Leonel.
Akimzungumzia
Tchetche kigogo mmoja wa Azam alisema: “Kuhusu Tchetche yuko sokoni
lakini wanaomhitaji wafahamu dau lake ni Dola 200,000.”
Katika
hatua nyingine, Azam itaanza maandalizi yake leo Jumatatu na wachezaji
wote wataanza mazoezi Uwanja wa Chamazi isipokuwa wale waliokuwa na timu
zao za Taifa.
Mmoja
wa maafisa wa El Merreikh ameliambia Mwanaspoti kuwa, klabu yake
ilikubaliana na Wawa kuvunja mkataba wake uliobakiza miaka miwili na
aondoke kama mchezaji huru kwani mwenyewe aliomba kuondoka.
“Wawa
tulikubaliana naye aondoke baada ya kutuomba kwani amecheza kwetu kwa
miaka mitano na kuitumikia klabu asilimia 96, sasa mtu mliyeishi naye
vizuri akiomba kitu lazima mumsikilize hivyo ameondoka kama mchezaji
huru.
“Lakini
katika kuondoka kwake ametuachia kasheshe hapa kwani mashabiki
wamekasirika, hawaelewi kilichotokea lakini hatukuwa na jinsi kwani Wawa
alituambia hata kama akibaki hana uhakika na uwezo wake utakavyokuwa,”
alisema kiongozi huyo.
Mwanaspoti
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni