LOGO

 
Simba SC leo wamepata ushindi wao wa kwanza katika michezo ya ligi kuu baada ya kucheza michezo 12 bila kupata ushindi wowote ule, michezo 6 katika msimu uliopita na michezo mingine 6 katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom.
Simba SC hii leo wameifunga Ruvu shooting goli 1-0 na kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza toka waifunge Ruvu shooting machi 2 katika uwanja wa Taifa goli 3-2.
Katika mchezo wa leo ambao ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko bila ya kufungana ambapo kwa Simba SC ni mara yao ya kwanza msimu huu kwenda mapumziko bila ya kupata goli na kisha kupata goli kipindi cha pili.
Simba SC walifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Yanga na mchezo kumalizika kwa sare bila ya kufungana.

Kama ilivyoada Simba SC waliutawala mchezo katika kipindi cha kwanza na huku wakitengeneza nafasi kadhaa za magoli ambazo walishindwa kuzitumia, wakati wa pinzania wao Ruvu Shooting wao wakifika mara chache langoni mwa Simba SC aambapo beki za Simba SC sambamba na kipa Ivo Mapunda waliondosha hatari zote.
Kipindi cha pili siku ya leo Simba SC walikuja kivingine kabisa kwani waliendelza kasi yao ya mchezo kinyume na michezo iliyopita ambapo katika kipindi cha pili kasi ya Simba SC huupunguwa na kuanza kuruhusu magoli.
Simba SC waliendelea kuwafanya Ruvu shooting waendelee kukaa nyuma huku wakiongeza kasi ya ushambuliaji.
Jitihada za Simba SC zilizaa matunda katika dakika ya 78 baada ya Emmanuel Okwi kuwaada mabeki wa Ruvu shooting na kumpasia Maguli ambaye shuti lake lilitemwa na kipa na mpira kumkuta Emanuel Okwi na bila ajizi Okwi akaiandikia Simba SC goli la kuongoza.
Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Ruvu shooting kufunguka kwa kusaka goli la kusawazisha kitendo ambacho kilipelekea Simba SC kutengeza na fasi mbili ambazo zingezaa magoli kama safu yake ya ushambuliaji ingekuwa makini.
Mpaka kipenga cha mwisho kina pulizwa Simba SC wakitoka na ushindi wake wa kwanza baada ya siku 252 kucheza bila ya kupata ushindi wowote ule.
Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Azam Complex wenyeji JKT Ruvu walifanikwa kuwafunga Ndanda FC goli 2-0.

MATOKEO YA WIKI YA 7 VPL

YANGA 2-0 MGAMBO SHOOTING
AZAM FC 2-1 COASTAL UNION
MTIBWA SUGAR 1-1 KAGERA SUGAR
STAND UNITED 1-0 MBEYA CITY
POLISI MOROGORO 1-0 T.PRISONS
JKT RUVU 2-0 NDANDA FC
SIMBA SC 1-0 RUVU SHOOTING

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top