MATOKEO LIGI KUU ENGLAND LEO JUMAPILI LIVERPOOL YACHAPWA TENA UGENINI SPURS YASHINDA KWA MBINDE
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Saa za Bongo
Jumapili Novemba 23
Crystal Palace 3 Liverpool 1
Hull City 1 Tottenham 2
LIVERPOOL, wakicheza Ugenini huko Selhurst Park Jijini London, waliongoza baada ya Sekunde 90 tu kwa Bao la Rickie Lambert lakini wakajikutwa wakibwagwa chali na kukung’utwa Bao 3-1 na Crystal Palace katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Palace walisawazisha Bao katika Dakika ya 17 kwa Bao la Dwight Gayle alienasa Shuti la Yannick Bolasie lililopiga Posti na kumrudia.
Kipindi cha Pili Dakika ya 78 Joe Ledley aliwapeleka Palace mbele 2-1 na kisha Dakika 3 baadae Frikiki ya Mita 25 ya Mile Jedinak ilitinga na kuwapa Palace Bao lao la 3.
Mechi hii imewaacha Wadau wa Liverpool wakihoji uchezaji wa Nahodha wao Steven Gerrard na Raheem Sterling ambao wameonyesha kufifia mno.
Kipigo hiki cha Leo kinawafanya Liverpool wawe wamechapwa Mechi 3 mfulilizo za Ligi na kushinda Mechi 1 tu kati ya 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 18 nyuma ya Vinara Chelsea.
Katika Mechi zao 2 zilizopita, Liverpool wametandikwa 2-1 na Chelsea na 1-0 na Newcastle.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann, Delaney, Ward, Bolasie, Jedinak, Ledley, Puncheon, Chamakh, Gayle
Akiba: Hangeland, Campbell, Zaha, Hennessey, Johnson, McArthur, Bannan. Liverpool: Mignolet, Manquillo, Lovren, Skrtel, Johnson, Allen, Gerrard, Coutinho, Sterling, Lambert, Lallana
Akiba: Brad Jones, Toure, Moreno, Lucas, Can, Borini, Markovic. REFA: Jon Moss
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni