Timu ya Southampton leo imeendelea kuwania nafasi ya kucheza ligi ya Mabingwa msimu ujao UEFA baada yka kutoka sare ya 1-1na Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu nchini England uliofanyika kwenye uwanja wa Vila Park.
Wenyeji Aston Villa ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa nahodha wake Gabriel Aghbonlahor katika dakika ya 29 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 1-0 hadi mapumziko.
Zikiwa zimebakia dakika 9 tu mchezo umalizike Nathaniel Clyne wa Southampton aliifungia timu yake goli la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi dakika ya 90 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo Southampton wanabaki nafasi ya pili wakijikusanyia pionti 26 mbele ya vinara chelsea wenye point 32 na Aston villa wanashika nafasi ya 16 wakiwa na pointi 12.
VIKOSI VILIKUWA HIVI
Aston Villa: Guzan, Hutton, Okore, Clark, Cissokho, Cleverley, Westwood, Sanchez, N'Zogbia, Agbonlahor, Weimann.
Subs: Bacuna, Cole, Richardson, Bent, Given, Lowton, Grealish.
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Alderweireld, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Tadic, Long, Mane, Pelle.
Subs: Kelvin Davis, Yoshida, Gardos, Cork, Mayuka, Reed, Targett.
Referee: Phil Dowd (Staffordshire)
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni