FIFA imetangaza Wagombea 10 kuwania Tuzo ya Puskas, Goli Bora la Mwaka, na upigaji Kura wake umeanza.
Mashabiki Dunia nzima wamekaribishwa kupiga Kura zao ili kumpata
Mshindi wa Tuzo hii ambayo hutolewa na FIFA kwa kushirikiana na Jarida
la France Football.
Magoli hayo 10 Bora yamependekezwa na Kamati ya Soka ya FIFA na
Washabiki wanatakiwa wapige Kura kupitia Mitandao ya FIFA na France
Football na Zoezi hili kufungwa hapo Desemba 1.
Siku hiyo hiyo Desemba 1, Magoli Matatu Bora yatangazwa na Washabiki
kupewa Nafasi nyingine kupigia Kura Goli Bora ambalo litashinda Tuzo ya
Puskas na Mshindi kutangazwa Januari 12 Siku ambayo pia Mshindi wa FIFA
Ballon d’Or, Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, atatangazwa.
Tuzo ya Puskas, Goli Bora la Mwaka, ilianzishwa kumuenzi Lejendari
Ferenc Puskás, Nahodha wa Timu ya Taifa ya Hungary katika Miaka ya 1950.
Hii itakuwa ni mara ya 6 kwa Tuzo hii kutolewa.
Kwa kuyaona Magol hayo 10 na kupiga Kura BOFYA HAPA:
http://www.fifa.com/ballon-dor/puskas-award/index.html
TUZO YA PUSKAS
WAGOMBEA 10:
Tim Cahill – 18 Juni 2014, Australia v. Netherlands, 2014 FIFA World Cup™ Diego Costa – 23 Novemba 2013, Atlético Madrid v. Getafe, Primera División (Spain) Marco Fabian – 15 Februari 2014, Cruz Azul v. Puebla, 1a División 2014 Clausura (Mexico) Zlatan Ibrahimovic – 19 Oktoba 2013, Paris St. Germain v. SC Bastia, Ligue 1 (France) Pajtim Kasami – 21 Oktoba 2013, Crystal Palace v. Fulham, Premier League (England) Stephanie Roche -20 Oktoba 2013, Peamount United v. Wexford Youths, BEWNL (Rep.Ireland) James Rodriguez – 28 Juni 2014 – Colombia v. Uruguay, 2014 FIFA World Cup™ Camilo Sanvezzo – 6 Oktoba 2013 – Vancouver Whitecaps v. Portland Timbers, MLS (USA/Canada) Hisato Sato – 8 Machi 2014 – Sanfrecce Hiroshima v. Kawasaki Frontale, J.League (Japan) Robin van Persie – 13 Juni 2014 – Spain v. Netherlands, 2014 FIFA World Cup™
Nyumbani
»
» Unlabelled
» HAWA NDIO WACHEZAJI WALIOTAJWA NA FIFA KUWANIA TUZO YA GOLI BORA LA MWAKA PUSCAS AWARD RVP YUPO RONALDO MESI OUT
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZILIZOSOMWA SANA
-
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupig...
-
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha mi...
-
Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzani...
-
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko...
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni