LOGO

 ARSENALvMANUNITED-LOGO
HII Leo Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ameongea na Wanahabari kuhusu Mechi yao ya Jumamosi na Arsenal huko Emirates na hasa hali ya Wachezaji wake Majeruhi ambao mwanzoni mwa Wiki walifikia 12 toka Timu ya Kwanza.
Akiongea huko Aon Training Complex, Carrington Jijini Manchester, Van Gaal alitoboa kuwa Angel Di Maria, David De Gea na Michael Carrick wako fiti kuivaa Arsenal.
Alisema: “Ni ngumu kusema kama wote wamerudi kwa sababu inabidi tusubiri hadi Mazoezi ya Ijumaa na kuamua. Falsafa yangu ni kuwa ufanye Mazoezi si chini ya Wiki moja na Kikosi kizima, vizuri hasa ni Wiki 2. Lakini kwa hali yetu, inabidi tuwaingize Wachezaji hao Kikosini hivi sasa.”
Alifafanua: “Di Maria amefanya mazoezi kawaida tu, hamna tatizo hapo lakini Shaw lipo. De Gea safi, hamna tatizo. Kwa Carrick inabidi tusubiri kidogo lakini yupo tayari kucheza.”
Kuhusu kuumia kwa Kiungo Daley Blind ambae alipata tatizo la Goti akiichezea Nchi yake Netherlands, Van Gaal amesema amewekewa sapoti kwenye Goti na atapimwa baada ya Siku 10 lakini hayupo katika hali mbaya kama ilivyofikiriwa.

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger ametoboa kuwa Majeruhi wake Olivier Giroud na
Mikel Arteta wako fiti kuivaa Manchester United Uwanjani Emirates Jumamosi kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Giroud hajacheza Mechi tangu Agosti alipovunjika Mguu kwenye Mechi waliyotoka Sare 2-2 na Everton na ilikisiwa kuwa atarejea Uwanjani mwanzoni mwa Januari.
Kuumia kwa Giroud kulimfanya Wenger akimbilie kumnunua Straika wa Man United Danny Welbesk Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho hapo Septemba Mosi kwa Pauni Milioni 16.
Akiongelea kuhusu Mechi ya Jumamosi, Wenger alisema: “Giroud na Arteta wanaweza kucheza. Ni uamuzi tu wako fiti kiasi gani. Lakini wanaweza kucheza.”

Uso kwa Uso
Arsenal v Man United
Mechi: 208
-Arsenal Ushindi 73
-Man United 87
-Sare 48

Vile vile Wenger alidokeza kuwa Mabeki wake majeruhi, Mathieu Debuchy na Laurent
Koscielny, wanaendelea vizuri na wameanza Mazoezi lakini itawachukua hadi Wiki 3 kuanza tena Mazoezi kamili ya Kitimu pamoja na wenzao.
Arsenal wataingia kwenye Mechi hii ya Jumamosi wakiwa Nafasi ya 6 Pointi 1 tu mbele ya Man United ambayo iko Nafasi ya 7.
Mara ya mwisho Arsenal kuifunga Man United ni Mei Mosi Mwaka 2011 Bao 1-0 Uwanjani Emirates kwenye Mechi ya Ligi na tangu wakati huo wamecheza Mechi 6 na kutoka Sare 2 tu na zote zilizobaki Man United kushinda ukiwemo ushindi wa kishindo wa Bao 8-2 hapo Tarehe 28 Agosti 2012.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top