KLABU zote za Ligi Kuu zikiwamo Simba na
Yanga zimetoa siku saba kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi kufanyia kazi mapendekezo yao ya kutokatwa asilimia tano
za mgawo wao wa wadhamini wa ligi hiyo vinginevyo watagomea ligi hiyo.Klabu za Ligi Kuu Bara zinapokea fedha
za udhamini Sh73 milioni kutoka Vodacom na Sh110 milioni kutoka Azam TV
ambazo asilimia tano yake ni Sh9.15 milioni na kwa klabu 14 za ligi hiyo
TFF itapata Sh128 milioni.Klabu hizo kupitia mwanasheria wao,
Damas Ndumbaro, amesema kuwa endapo mapendekezo yao yatashindwa
kufanyiwa kazi kwa siku walizotoa basi watachukua hatua mbalimbali ili
kupata haki yao ikiwamo kufungua kesi ya malalamiko katika Shirikisho la
Soka la Kimataifa (Fifa).Pia Ndumbaro alisema wataungana kugomea
ligi hiyo hadi watakapopata haki yao, lakini watahakikisha wanamfikisha
mahakamani yeyote atakayebainika kukata makato hayo kinyume na
utaratibu.“Rais amesisitiza makato haya ya
asilimia tano kinyume na taratibu kwani waliopitisha mchakato huu siyo
klabu zenyewe, watu wa bodi waliokuwapo katika kikao hawakukubali makato
haya ndiyo maana hadi leo TFF hawajatoa taarifa za kikao hicho,”
alisema Ndumbaro.
Juzi
Alhamisi Malinzi alitoa tamko kwamba ni lazima klabu zikatwe asilimia
tano kutoka kwa wadhamini wao ambazo ni kwa ajili ya mfuko wa maendeleo
ya soka la vijana na Ligi ya Wanawake.Ndumbaro alisema wanaikaribisha TFF
mezani ili kujadili mchakato huo lakini msimamo mwingine kama Malinzi
hatabadili msimamo ni kugomea kuvaa jezi za Vodacom ambao ni wadhamini
wao. Mwanasheria huyo alienda mbali kwa
kusema wametoa ombi la kukaguliwa kwa matumizi ya fedha TFF tangu
uongozi wa Malinzi ulipoingia madarakani Oktoba 2013.Ndumbaro alisema kuwa wateja wake ambao
ni klabu 14 za Ligi Kuu Bara wanalalamikia kukatwa asilimia tano kutoka
Vodacom na Azam TV kinyume na makubaliano ya mkataba wao na haraka
wanataka kukaa meza moja na Malinzi ili kumaliza tatizo hilo.“Tumeonyesha nia ya kutokuwa na imani na
Malinzi pamoja na uongozi wake kwa jinsi wanavyosisitiza mchakato huu.
Tutaomba mkutano mkuu wa dharura ambapo wanachama ndiyo walioichagua
Bodi ya Ligi na wana uwezo kuifanya bodi iwepo ama isiwepo ili kupiga
kura za kusudio la kutomwamini Malinzi,” alisema Ndumbaro.Ndumbaro alisema TFF wana mgao wao
wanaupata kutoka Vodacom na Azam TV kwa ajili ya mambo ya uendeshaji
hajui ni kwa nini wanaendelea kuzinyonya klabu.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni