Na Boniface Wambura,
Kikosi
cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua
jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa
Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.

Wachezaji
wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana
(Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) kwa nyakati tofauti.
Kikosi
hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10
jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho
kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Wachezaji
walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich
Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon
(Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg,
Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed
Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve
Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne
63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia
Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na
Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean
Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef,
Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS
Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
Wakati
huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle
Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka
huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni