
Mchezaji wa Simba FC inayoshiriki Ligi Kuu Uganda, Fahad Musana amefariki dunia ghafla wakati akiwa kwenye banda la video kushuhudia mechi ya Ligi Kuu England kati ya Manchester City na Chelsea juzi.

Kwa mujibu wa mtandao wa kawowo.com, Musana (24), alianguka sekunde chache tu baada ya Frank Lampard kuifungia Man City bao la kusawazisha katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1. Musana ni shabiki mnazi wa Chelsea. Kilichoshtua ni kwamba Musana alicheza mechi ya ligi dhidi ya Entebbe kwenye Uwanja wa Nakivubo Jumamosi iliyopita na timu yake iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Imeelezwa kwamba juzi Musana alifanya mazoezi na wenzake na kupata nao mlo wa mchana kabla ya kwenda kutazama mechi ya Manchester United na Leicester City kwenye banda hilo lililopo Bombo Mjini na baadaye akasubiri pia mechi ya klabu yake ya Chelsea. Musana alionekana kuwa na furaha wakati Chelsea ilipokuwa mbele kwa bao la Andre Schurrle, lakini baada ya Lampard kusawazisha tu alianguka na kufariki dunia. Maiti yake ilipelekwa katika Hospitali ya jeshi ya Bombo.
Fahad Musana | |
---|---|
Tarehe ya kuzaliwa | 12 october 1990 iganga, Uganda |
Tarehe aliyofariki | 21 de septiembre de 2014 (23 años) Lugazi, Uganda |
Taifa | ![]() |
Nafasi anayocheza | Beki/Defender |
Alijiunga na Simba | 2010 |
Clabu anayochezea | Simba FC |
Hadi mwaka | 2014 |
Alifariki akiwa mchezaji wa | Simba FC |
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni