STRAIKA Mrundi Didier Kavumbagu wa Azam FC amepiga mabao mawili katika mechi ya kwanza ya ligi akiwa na timu yake lakini ameingia kwenye rekodi ya kufunga bao la kwanza la mapema msimu huu.
Alifanya hivyo Azam ilipoichapa Polisi Morogoro mabao 3-1. Kavumbagu amefunga bao dakika ya 14, kama ilivyokuwa kwa Ramadhani Pera wa Mgambo Shooting ambaye pia alifunga bao katika dakika hiyo ya 14.
Katika viwanja vingine, Mkwakwani Tanga, Mgambo Shooting iliifunga Kagera Sugar bao 1-0 na bao la Maafande hao lilifungwa na Ramadhani Pera dakika 14.
Katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Mtibwa iliifunga Yanga mabao 2-0 na bao la kwanza lilifungwa na Mussa Hassani ‘Mgosi’ dakika ya 16 na la pili lilifungwa na Ameir Amour dakika ya 82.
Mechi ya Shinyanga iliyocheza Uwanja wa Kambarage Ndanda ilishinda mabao 4-1.
Mabao ya Ndanda la kwanza lilifungwa na Paul Ngalema dakika ya 15, Nassor Kapama alifunga la pili dakika 22, Gidion Braun alifunga la tatu dakika ya 35 na la nne lilifungwa na Elius Ndokezi dakika 90.
Bao la Stendi lilifungwa dakika ya 28 na Kamana
Salum.Mechi ya Uwanja wa Mabatini ambayo Tanzania Prisons iliifunga Ruvu Shooting mabao 2-0. Mabao ya Prisons yalifungwa na Lawrian Mpalile dakika ya 16 na Jacob Mwaitalile dakika ya 59.
Uwanja wa Sokoine Mbeya, Mbeya City ilitoka sare kwa kumaliza mechi bila ya kufungana na JKT Ruvu.
MWANASPOTI
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni