LOGO

Klabu ya soka ya Yanga SC imeenda kuweka kambi Visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa ligi kuu bara msimu ujao pamoja na mihuano ya kimataifa  ikiwa na msafara wa watu 35 ambao wacheazaji ni,27, chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo umewasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Maximo na kikosi chake wamefikia katika hoteli ya kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha na watakuwa huko kwa siku 10 kabla ya kurejea Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi huu.

Kikosi cha Yanga kitakua kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani, Chake Chake wakati Alhamisi watacheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya  Chipukizi ya Pemba.
Yanga SC itacheza mechi tatu za kirafiki na timu za Pemba na Unguja na baadaye kurejea Dar es salaam kwa michezo mwili ya kimataifa kabla ya kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani Septemba 13, 2014.
Wachezaji waliopo kambini Pemba ni makipa; 
Juma Kaseja, Ally Musatfa ‘Barthez’ na Deogratias Munish ‘Dida’, mabeki Juma Abdul, Salum Telela, Oscar Joshua, Edwad Charles, Amos Abel, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo ni Mbuyu Twite, Said Juma, Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Hamisi Thabit, Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Nizar Khalfan na Andrey Coutinho, wakati washambuliaji ni Geilson Santos ‘Jaja’, Said Bahanuzi, Jerry Tegete, Hamisi Kiza na Hussein Javu. 
Benchi la Ufundi linaoongozwa na Maximo, wasaidizi wake, Leonardo Neiva, Salvatory Edward, kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Mchua Misuli Jaco Onyango na Mtunza Vifaa, Mahmood Omar ‘Mpogolo’.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top