LOGO

 2015 AFCON

Chama cha soka cha nchini Rwanda kimekata Rufaa kwa shirikisho la mpira wa miguu Africa CAF kufuatia maamuzi ya kuiondosha kuwania tiketi ya kufuzu kwenye mashindano ya Africa yatakayo fanyika moroco mwakani 2015 hayo yamesemwa na mkuu wa chama hicho cha soka Rwanda  Olivier Muhindahabi.
Rwanda wanatarajiwa kupeleka rufaa hiyo leo jumanne usiku kwenye bodi ya rufaa ya CAF dhidi ya tuhuma zilizotolewa na CAF siku ya tarehe 17 Jumapili kwa kumchezesha mchezaji mwenye uraia wa nchi mbili na kusababisha kutolewa mashindanoni na kamati ya CAF 
Muhindahabi amesema wamekutana na wanasheria wao kujadili hili pamoja na kusoma vipengele hivyo vilivyo sababisha wakatolewa na kabla ya kutoa maamuzi ya kukata rufaa ndani ya masaa 48 
Tulipokea email ikionyesha kuwa timu ya Rwanda imeondoshwa mashindanoni ila ghafla tukafikiria kukata rufaa kwa sababu sio haki na sio sawa baada ya muda mfupi kuondolewa nafasi yetu imechukuliwa na CONGO DRC
Nafikiri tunauwezo wa kufanya maamuzi na tukakubaliwa kwasababun sisi sio sehemu ya mchezaji huyo kubadilisha jina lake amesema Muhindahabi.
Rwanda ilikuwa kundi Apamoja na mataifa ya Nigeria, South Africa and Sudan.  
Chama cha soka cha Congo ndio kiilishtaki Rwanda kwa kumchezesha mshambuliaji mzaliwa wa kongo  Dady Birori  July 20, ndani ya  Pointe-Noire kuwa mshambuliaji huyo anatumia majina mawili tofauti.
Katika kauli iliyotolewa jana na kamati ya mashindano ya AFCON imesema Birori amesajili kwa jina la Agiti Tady Etekiama na pia kutumia umri tofauti kwenye klabu yake ya AS VITAL ya CONGO DRC 
Etekiama alikuwa shujaa wa Rwanda katika mechi ya makundi walipoilaza Libya mabao 3-0 mjini Kigali ambapo alifunga magoli matatu na kuivusha Amavubi hatua inayofuata ambapo watacheza na Congo
Mshambuliaji huyo anatumia passport mbili zenye majina tofauti ya kwanza ni ya Rwanda yenye jina la Daddy Birori aliyezaliwa December 12, 1986, na yapili ni ya Congo inayomtambulisha kama Agiti Tady Etekiama, aliye zaliwa December 13, 1990.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top