TAREHE.14.08.2014.
UTANGULIZI.
Ndugu wanaHabari,
Mtakumbuka kwamba Tarehe 9.08.2014, katika vyombo mbali mbali vya habari na
mitandao ya kijamii imeripotiwa Taarifa ya TUNDU LISSU na waliokuwa
MADIWANI wa shinyanga mjini baadae wakahamia CCM, pamoja na Tuhuma
nyingine kwamba kuliwahi upangwa mpango wa KUILIPUA HELKOPTA iliyowabeba WILBROD SLAA na JOHN MNYIKA ili wafe,
Na wanasema miongoni mwa waliohusika kufanya mkakati huo ni Ndugu HABIBU MCHANGE, ambaye ni Mimi.
Japo
kuwa hii si habari ya kwanza ya kipuuzi inayotolewa na viongozi wa
CHADEMA ikinihusisha mimi ama moja kwa moja au la, tangu baada ya
mgogoro wangu wa kisiasa ndani ya CHADEMA may 2011.
Na habari nyingi kati ya hizo nimeamua kuzipuuzia, leo ninaomba kusema kidogo ili kuweka kumbukumbu sawa na sahihi.
KUHUSU KUILIPUA HELKOPTA.
Pamoja na kwamba hekaya hii ni ya kipuuzi,
Haingii
akilini hata kidogo kwamba mimi Habibu Mchange Nimepanga na CCM na
naibu waziri kuilipua helkopta ambayo ingewabeba Slaa na Mnyika.
Upuuzi
huu ulioratibiwa na Tundu Lissu, ni uthibitisho wa kushindwa na
kuporomoka kisiasa kwa kasi ya ajabu kunakoikabili CHADEMA kwa sasa, na
kujiokoa kwenye hilo wanaanza sasa kutengeneza tuhuma za kitoto namna
hii zisizokuwa na kichwa wala miguu ili kupata huruma ya wananchi.
Ninawezaje kupanga mikakati ya kulipua helkopta, ili iwe nini?
Kwangu mimi kwa sasa Slaa ni miongoni mwa wanansiasa dhaifu waliowahi kutokea kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania.
Slaa ameshajiishia, nimlipue ili iwe nini?
Mtu
aliyeishiwa ushawishi kama yeye, kiasi cha kushindwa kumshawishi hata
mke wake aliyemzalia watoto wawili, anawezaje kuwa Tishio na kupangiwa
mikakati ya kulipuliwa?
Nasema
siwezi kufanya ujinga wa namna hii na hata kama angekuwa tishio
kisiasa, si hurka yangu kujihusisha na matukio ya KIGAIDI namna hii.
CHADEMA NA MAUAJI / UJANGILI
SLAA,
LISSU, MBOWE, MNYIKA, LEMA na CHADEMA ndio mabingwa wa matukio ya
KIGAIDI na utoaji roho za wenzao, hasa pale wanapokuwa wametofautiana
misimamo na mitazamo ndani ama nje ya Chama. Tafadhali wasitafute mtu wa
kushiriki naye dhambi za mauaji waliyoyatenda na wanayoendelea kutenda.
Dunia
Nzima inajua kwamba watu hawa wameshiriki kikamilifu kumuondoa DUNIANI
aliyekuwa makamu mwenyekiti wa chama CHACHA ZAKAYO WANGWE, Hii haina
ubishi kwamba, MBOWE, SLAA na MNYIKA walijaribu mara kadhaa kutaka
kumuua CHACHA WANGWE kwa kutumia sumu na kushindwa mpaka walipofanikiwa
kumuua kwa ajali ya kutengeneza tarehe 28.7.2008 wakimtumia kijana
ambaye Dunia nzima inamjua.
Na Mungu anawaumbua, sasa wanahaha, leo nitaongeza ushahidi kwenye mauaji ya haya.
Angalia Mfano huu.
Tarehe
28.05.2008, JOHN MNYIKA, akiwa mkurugenzi wa vijana CHADEMA taifa
kipindi hicho, alitukutanisha mimi Habibu Mchange, Marehemu Regia Mtema,
Deus Mallya na vijana wengine wawili, ofisini kwake ambapo kwa sasa
ofisi hiyo inatumika kama ofisi ya Naibu katibu mkuu, pamoja na mambo
mengine tukajadiliana namna ya kulieneza Baraza la Vijana na kuongeza
wanachama wengi vijana, na tukapeana majukumu, kwamba mimi nishuhulike
mashuleni na vyuo vikuu vishiriki kama DIT na CBE, kwa kuwa nilikuwa na
mahusiano na watu wengi huko, DEUS MALLYA alipewa jukumu lingine
sambamba na marehemu REGIA MTEMA, lakini kwa pamoja tukawa kwenye kamati
ambayo mwenyekiti wetu ni JOHN MNYIKA mimi nikiwa mjumbe kutokea wilaya
ya Temeke.
Tarehe 28.07.2008 usiku, CHACHA WANGWE aliuawa PANDAMBILI DODOMA, na mtu aliyekuwepo kwenye tukio hilo ni DEUS MALLYA, nini kilitokea?,
Tarehe 29.07.2008 saa tano asubuhi, JOHN MNYIKA alifanya
mkutano na Waandishi wa HABARI, akimkana DEUSI MALLYA kwamba CHADEMA
haimtambui, na kwamba SERIKALI iwajibike kuueleza UMMA kwamba DEUS
MALLYA ni nani na amewezaje kuwa Dereva wa Chacha wangwe ambaye ni
Mbunge huku chama kikiwa hakimtambui DEUS MALLYA wala hakijawahi kumuona
mahala popote na kwamba akamatwe Haraka na hatua kali dhidi yake
zichukuliwe Haraka.
Maana yake nini?. Ni kwamba MNYIKA na CHADEMA wamemkana DEUS MALLYA kimkakati ili kukiondoa chama kwenye ushahidi wa mauaji ya kiongozi wake mkuu msaidizi.
Jiulize
maswali, kwanini MNYIKA alimkana DEUS MALLYA aliyekuwa sio tu rafiki
yake lakini mshirika wake mkuu kwenye harakati za ujenzi wa chama?.
Kama hawahusiki Kumuua WANGWE kwanini waogope kiasi cha kumkana mwanachama mwandamizi wao?.
Na kwanini Mbowe alitumia nguvu kubwa sana kuhakikisha Deus Mallya anashinda Rufaa na anafutiwa Kesi?.
Na kwanini Mnyika na Mbowe walimuomba Msamaha Deus Mallya baada ya Kutoka Gerezani kwa kitendo chao cha Kumkana baada ya tukio la mauaji?.
Watanzania wanatambua kwamba
MBOWE, LISSU, SLAA na CHADEMA tumeshiriki kikamilifu kutengeneza
matukio ya hatari yenye kuonyesha nchi haitawaliki na upinzani hasa
CHADEMA inanyanyaswa na Dola na polisi ili chama kizidi kupata umaarufu
wa kisiasa.
Hii
ndio maana MBOWE na SLAA wamemtuma kijana mmoja mrefu, mweupe mwenye
mazoea ya kufuga nywele nyingi aliyechanganya uraia wa Tanzania na
German(ama nchi nyingine ya ulaya)(sitamtaja jina kwa sasa. Mbowe na
CHADEMA wanamfahamu) ambaye kwa sasa ni kiongozi katika ngazi ya wilaya
mkoa mmoja wa kaskazini kutekeleza mpango wa mauaji kwenye matukio
makubwa ya mikutano ya kisiasa hasa inayohusisha vurugu kati ya chadema
na polisi na kumuandaa mtu mmoja maalum kwa ajili ya kupiga picha
matukio hayo na kusambaza haraka mitandaoni huku mwengine akichukua
VIDEO.
Kijana
huyu ambaye ni Swahiba wa MBOWE na LEMA, ameweza kutekeleza kazi yake
hii Tarehe 05.2.2011 pale ARUSHA kwa kwaua watu kadhaa na kisha umma
kuaminishwa kwamba mauaji yale yalifanywa na polisi walipokuwa
wanawazuia waandamanaji. Mpaka sasa polisi inahangaika kujinasua kwenye
matukio haya ya kutengeneza. Mimi, Mbowe,Slaa, Lissu na Mnyika
tunafahamu kila kitu.
Kijana Huyu kwa maelekezo ya MBOWE kupitia kwa SLAA na MNYIKA ili kuwatisha wakazi wa IGUNGA, usiku wa tarehe 9.9.2011 Wakitumia gari namba T587 AZJ TOYOTA LANDCRUISER VX mali
ya FREEMAN AIKAEL MBOWE, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na
Kiongozi mkuu wa Upinzani Bungeni akiwa na HEMEDI SABULA, HENRI KILEWO
na JOHN HECHE wakiwa na vijana kadhaa wenyeji wa IGUNGA walimteka na
kumtesa sana kijana MUSSA TESHA na kisha kumpeleka Pori la MSITU WA HANI HANI na kummwagia TINDIKALI Usoni, ili eti vijana wengine waogope kuiunga mkono CCM na vyama vingine.
Na
haya yote yalifanywa kwa maelekezo ya SLAA na MBOWE na ndio maana baada
tu ya Tukio, Slaa alimuagiza mkurugenzi wa kampeni na uchaguzi
aidhinishe malipo ili mkurugenzi wa fedha alipe na vijana hawa
wakapelekwa MWANZA na kuhifadhiwa kwenye Hotel ya MAGNUM kwa
zaidi ya Mwaka mmoja. Wakiendeshwa na Dereva mmoja maarufu sana wa
chadema, sitamtaja kwa leo kwa kuwa alikuwa anatii maelekezo ya viongozi
wake.
Mauaji
na Mateso yote ya Kijangili yaliyofanywa IGUNGA na ARUMERU yaliwekwa
kwenye mpango mkakati wa CHAMA na kupitishwa na KAMATI KUU YA CHAMA.
Ni hatari sana kikao kikuu cha chama kuhalarisha mauaji. Nimeambatanisha na sehemu ya ripoti na mkakati huo wa mauaji.
U wapi sasa uzalendo wa viongozi hawa?, uko wapi uzalendo wa mbowe, uko wapi uzalendo wa Slaa, Lissu na wahuni wenzao wengine?. HAWA NI WAUAJI TU KAMA WAUAJI WENGINE. NA WALAANIWE
MBOWE, SLAA na LISSU, wanajua namna gani walivyomtuma muuaji wao huyu aliyesomea kwa kushiriki kumuua mtu asiye na hatia pale morogoro tarehe 27.08.2012 ndugu ALLY ZONA aliyekuwa muuza magazeti pale msamvu, leo hii Dunia nzima inajua kwamba Ally aliuawa na polisi, ila MBOWE, SLAA na CHADEMA wanaujua ukweli halisi.
Wakati Dunia Nzima Leo inaamini kwamba polisi wa F.F.U walihusika kumuua David Mwangosi tarehe2.9.2012 pale Nyororo Iringa, MBOWE, LISSU, MNYIKA na SLAA wanaujua
ukweli, wanajua ni namna gani mchezo huu ulipangwa, namna gani mpiga
picha aliandaliwa, namna gani taarifa za awali zilisambazwa na namna
gani mlipuaji alifika eneo latukio na kutekeleza kazi yake maalum na
baadae kuondoka kwa utaalamu wa hali ya juu, wanafahamu fika. Na kwenye
hili pia mpaka sasa polisi wanahangaika kujinasua, lakini bado
wamekwama.
MBOWE, SLAA, LISSU na CHADEMA huku wakishangilia, waliwaagiza vijana wao wampige, na kumdharirisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ndani ya kikao cha kamati kuu Ndugu SHAABAN MAMBO tarehe 3.1.2014 ukumbini MBEZI GARDEN
CHADEMA NI WATEKAJI.
Tarehe 6.1.2014. SLAA aliwaagiza HEMEDI SABULA, MEDI, MWAKYEMBE na REDBRIGADE kwenda kufunga OFISI YA MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE JOSEPH YONAH , na ilipofika SAA TANO USIKU wakamfuata mtaani kwake, wakamteka, wakampiga sana kisha wakaenda kumtupa UNUNIO baada ya kudhani kwamba wameshamuusa.
Na
wakati wote wakimpiga na kumtesa walisema wapo Tayari kumsamehe na
kumuachia ikiwa tu atakubali kukiri na kurekodiwa kwamba ametumwa na
Zitto Kabwe, Mwigulu Nchemba, Usalama wa Taifa kukihujumuCHADEMA. Jambo ambalo si kweli na si sahihi.
Tulipomuokota
UNUNIO alipofika Hospitali, SLAA aliwatuma vijana wake kwenda kuiba
PF3- na kwa njia walizozijua mpaka sasa PF3 ya YONA ipo mikononi mwa
SLAA ambaye kwa kweli ni Muuaji na wala hana huruma.
SLAA akishirikiana na watesi wenzake walimteka, kumtesa na kumjeruhi ndugu JOHN MARWANYANCHABO, kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 6.02.2014 mpaka tarehe 9.02.2014 na
kumfungia ndani ya chumba cha ofisi ya CHADEMA wilayani BAGAMOYO huku
wakimlazimisha kusema maneno ya hovyo kwamba ametumwa na CCM na ZITTO
kuihujumu CDM na mambo mengine.
Sasa
kunihusisha mimi naulipuaji wa helkopta ya Slaa na Mnyika helkopta
ambayo waliopanda wana utaalam wa ujangili ni kunikosea heshima. Na kwa
kweli kwenye Hili Mwenyezi Mungu wa Rehema atawalaani.
KUHUSU MADIWANI KUHAMIA CCM.
Kuniambia kwamba mimi ndiye niliyewashawishi wahame CHADEMA na wahamie CCM ili kisha wahamie ACT ni utoto ulipitiliza.
Pamoja na kwamba nina mahusiano mazuri sana na Diwani SEBASTIAN PETER – OBAMA.
Ninafahamu kwamba OBAMA alibakisha wiki mbili afukuzwe uanachama wake wa chadema, kama mnyika alivyotangaza pale shinyanga,
Na
ninafahamu kwamba OBAMA ni miongoni mwa vijana wanaochukizwa na UBAGUZI
wa wazi unaoendelea ndani ya chama, na mimi nayeye uhusiano wetu
umeimarishwa hasa na misimamo hiyo.
Hivyo
ninakumbuka namna ambavyo alikuwa anapambana kuhakikisha haki yake ya
kutokufukuzwa inapatikana, hii ni yeye na diwani wa kahama ndugu SHABAN
BOBSON
Na
hata alipojiunga na CCM sikushangaa sana nilimpongeza kwa uamuzi wake
kwa kuwa alikuwa kwenye political frastruations nay eye ni muandishi wa
hatma yake mwenyewe.
Kusema
kwamba mimi nilimshawishi ahamie CCM anaongopa, na anaongopa pengine
anataka kuwaaminisha kwamba viongozi wengi wa CHADEMA wana uwezo mdogo
sana, kiasi kwamba wanaweza kushawishiwa na mtu ambaye siyo mwanaCCM ili
wao wajiunge CCM nay eye akabaki kutokuwa mwanaCCM.
Lakini
pia OBAMA anajaribu kuonyesha namna ambavyo viongozi wetu wa upinzania
wasivyokuwa na misimamo, kama jana alijiunga na CCM na SLAA akatangaza
hadharani kwamba huyo ni msaliti na kwamba angefukuzwa muda mchache, leo
karudi CDM anaitwa kamanda na mzalendo. Viongozi wa namna hii ikitokea
chama kikashinda dola wanaweza wakarubuniwa zaidi na zaidi na kujikuta
wanauza nchi kwa ahadi na matarajio ya kitoto
Lakini
pia nina fahamu kwamba OBAMA na mwenzake wapo kwenye UJIRA, wamelipwa
ama kununuliwa wafanye wanachokifanya ili kunjusuru uhai wa CHADEMA,
Na
hili ni azimio halali la kikao kati ya MBOWE, SLAA na viongozi wengine
kilichoketi DODOMA wakati wa Bunge la Bajeti, ambapo pamoja na mambo
mengine, CHADEMA imeadhimia kuwanunua viongozi na wanachama wote
wanaowapinga. Tayari wamefanikiwa kwa OBAMA.
Leo
hii Benson Kigaila ametumwa na SLAA kigoma kununua viongozi wengine
watoe matamko kama ya OBAMA, na JOHN MREMA yupo TABORA anazunguka
wilayani kugawa pesa ili waseme watakayoyasema, Henry Kileo na Kigaila
kwa pamoja wamemuhakikishia Joseph Yonah wa Temeke kwamba iwapo
atajitokeza hadharani kusema kuwa alikuwa anatumiwa na ZITTO ama na CCM
kupitia Mimi basi MBOWE na SLAA watabadilisha maisha yake na kumuahidi
donge nono. Tumefanikiwa kuwarekodi wakiongea ujinga huu.
Kwa
hiyo sina shaka kwamba madiwani hawa wanalipa walichokula, kwa hiyo ni
wakati wao kuendelea kubwabwaja, ukikubali kula cha mtu ukubali pia
kuliwa.
Ila
wawasaidie tu kuwaambia watanzania kama yale waliyokuwa wanayalalamikia
kutendeka ndani ya chadema siku chache nyuma kama tayari yametatuliwa
au bado?. Na kwamba Ufisadi wa mbowe waliousema Tayari umeisha ama
bado?, kwamba ubadhirifu wa SLAA waliousema Tayari umekoma au Bado?,
kwamba mauaji ya mbowe kumuua shelembi wa shinyanga kama walivyosema
yamebadilishwa ama bado?.
KUHUSU LEKADUTIGITE NA NSSF
Kila mara Lissu amekuwa akijitahidi kupambana na zitto hata katika maeneo asiyoyaweza.
Mimi
habibu Mchange, nimekuwa mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Lekadutigite, kampuni iliyoundwa na wasanii wa kigoma, na haijawahi
kutokea hata siku moja zitto ama kampuni kuhongwa pesa kiasi chochote na
NSSF na kwamba Lekadutigite walitengeneza wimbo ambao ni Tangazo
linaloitangaza NSSF na kupewa milioni 21 kama gharama za Tanzazo hilo na
hili ni kwamba wasanii hawa walijitolea walipaswa kulipwa hata milioni
900 kulinganisha na ukubwa wa kazi waliyofanya na ukubwa wa wasanii
husika, na maelezo mengine kuhusu malipo ya Nssf na lekadutigite tayari
Nssf wenyewe wameshayatolea ufafanuzi.
UNAFIKI WA LISSU.
· Lissu
anasema pesa za NSSF ndizo zilizotumika kulipa hao madiwani. NI UWONGO –
LEKADUTIGITE na NSSF mkataba wao wa kazi ni January mpaka February 2013
na walikabidhi kazi kisha wakatumbuiza Arusha mbele wa Makamu wa Rais
· Niliacha kazi LEKADUTIGITE April 2013 ili kuendelea na siasa hasa kuandaa jimbo langu la uchaguzi la kibaha mjini
· Zitto na baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waligombana mwishoni mwa 2013 na mahakamani ni mwanzoni mwa 2014
· ACT imeanzishwa mwezi may 2014, wakati hao madiwani wameshaondoka kitambo CHADEMA
Kumuhusisha
Zitto na mambo haya ni kuweweseka kwa kiwango cha juu kwa watu hawa.
Wao walishamfukuza zitto, wakasema hana impact, sasa yanini wanahangaika
naye?, kwanini hawalali wanaweweseka naye?, kwanini wanajihami?,
Hawajiamini?, kwanini wanakiogopa kivuli chake?,
Waache kumfuata fuata na waendelee na mambo yao.
Wajifunze kwa Zitto kukaa kimya na kuendelea na Maisha.
Lissu namshauri aache ubinafsi na ubabaishaji.
Dunia
nzima inafahamu kwamba alikula milioni 250 za wafadili kwenye shirika
lao la kiraia na shirika likafia hapo hapo nay eye kwenda kujenga
ghorofa pale tegeta.
Lissu hawezi kuwa kama zitto, zitto ni zitto na lissu ni lissu. Ninamshauri apunguze kukubali kuchukuliwa kama zezeta.
LISSU
ni MBINAFSI ALIYEPITILIZA na UBINAFSI WAKE ndio umemfanya mpaka
alipoombwa kushauri namna bora ya kupatikana kwa wabunge wa viti maalum
kama mwanasheria wa chama, akaweka sharti na kuhakikisha kwanza Dada
yake CHRISTINA LISSU anakuwa Mbunge wa Viti
maalum, na ndio maana dada yake alikuwa MBUNGE wa viti maalum wa
chadema kwanza kabla ya kuwa MWANACHADEMA. Alipelekewa kadi ya CHADEMA
bungenidodoma baada ya kula kiapo cha ubunge.
LISSU
NI MROPOKAJI ALIYEKUBUHU, na wote mnafahamu namna alivyotumika kuropoka
upuuzi kuhusu watu na taasisi mbali mbali na sasa CHADEMA wanajifanya
kuungana nao
Ni
lissu ndiye ndiye aliyemtukana na kumdhihaki Prof. BAREGU na kutaka
ajitoe kwenye chama ama abaki tume ya katiba kwa kuwa Tume haina weledi
Ni
lissu ndiye aliyemzihaki JOSEPH WARIOBA na kusema kwamba anaendesha
tume ki CCM CCM na kwamba CHADEMA haiungi mkono kitakachotolewa na Tume.
– leo LISSU na CHADEMA wamekuwa makwapani mwa TUME na WARIOBA
Aliwakashifu
CUF akawaita WAKE WA CCM, akawakashifu NCCR na MBATIA wao, akawakashifu
MAASKOFU na MASHEIKH akawakashifu wazanzibar. Leo aibu ya CHADEMA
imefichwa na CUF na NCCR-MAGEUZI.
Aache kuwa mnafiki wa kisiasa.
CHADEMA INAKUFA KWA KASI
Mwisho,
Yanayoendelea kutokea kwenye chadema leo ni kielelezo cha chama Kufa kwa kasi ya ajabu.
Watanzania tumewaongopea vya kutosha sana, tumetengeneza matukio vya kutosha sana, na tumewalaghai watanzania vya kutosha sana.
Sasa
hakuna uwongo mpya tunaoweza kuwapa, hakuna tukio jipya tunaloweza
kulitengeneza, tumeamua kujitekenya wenyewe halafu tunacheka wenyewe.
Hii ni ishara ya kudidimia kwa chama
Wazee wetu wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu, na ukitaka kuruka uagane na nyonga.
Kwa
kuwa tulikubali kujenga chama kwa kutegemea mtaji wa uwongo, na chama
kimeamua kufa kwa kutumia uwongo huo huo, mwisho wa siku jamii
itatucheka kwa kuwazoesha uwongo.
Nitaendelea
kusimamia kweli na haki daima Dumu. Nitaendelea kulilinda na
kulisimamia Taifa langu milele. Na nitaendelea kupiganian demokrasia ya
kweli kila siku
Mungu ibariki Tanzania
‘’SIO MAKOSA YANGU, MAKOSA LABDA YA KAZI’’
Habibu Mchange
0762178678/0658178678
‘’The Freedom Is Not Free’’
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni