Kwa matokeo hayo, KMKM inakamilisha mechi nne za kundi A ikiondoka na pointi mbili ilizovuna kwenye sare ya 1-1 mara mbili na Atlabara ya Sudan Kusini na Adama ya Ethiopia, huku mechi nyingine ikifungwa 4-0 na Azam ya Tanzania Bara.
Sibomana alitumia mwanya wa wachezaji wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo kutopanga ukuta wao vizuri na kumtungua kipa, Mudathir Khamis aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa kazi nzuri leo.
Kocha wa KMKM, Ally Bushiri ‘Bush’ alifanikiwa kuidhibiti Rayon kwa mfumo wa 4-5-1 na kufanya mchezo uwe mgumu kwa wenyeji- ingawa mvua ilipunguza ladha yake.
Mvua iliongezeka dakika ya 30 na Uwanja ukajaa maji, kiasi cha mpira kushindwa kutembea, lakini refa Muhabi Alex wa Uganda, hakujali hilo na ngoma iliendelea kupigwa.
Wakati wa mapumziko watu waliingia na mafagio kuondoa maji kwenye Uwanja huo wa nyasi bandia pamoja na gari maalum dogo mfano wa trekta.
KMKM waligoma kuendelea na mchezo katika hali hiyo, lakini wakashinikizwa na kukubali kwenda kumalizia dakika 45 ambazo ziliwamaliza pia kwa kufungwa bao la SIbomana.
Pamoja na kufungwa, KMKM walipoteza nafasi za wazi za kufunga zisizopungua tatu, moja Maulid Ibrahim ‘Kapenta’ aligongesha mwamba kipindi cha kwanza.
Katika mchezo uliotangulia wa kundi hilo, Atlabara ilitoka sare ya 1-1 na Adama, wakati mchezo wa Kundi C, wenyeji wengine, Polisi walishinda 3-1 dhidi ya Benadir ya Somalia.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B kati ya na wenyeji wengine APR watakaomenyana na Gor Mahia ya Kenya na Atletico ya Burundi na Telecom ya Djibouti, wakati Kundi C El Merreikh ya Sudan itakipiga na mabingwa watetezi, Vital’O
Adama City na Azam, Rayon na Atlabara, wakati Kundi B Telecom itamenyana na Gor Mahia na KCC na APR.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni