LOGO


Mahakama ya Usuluhisho Michezoni CAS, kesho  Alhamisi Agosti 14 itatoa uamuzi wa Rufaa ya Luis Suarez kupinga Kifungo cha Miezi Minne kwa kung’ata Meno Uwanjani, Mkuu wa FA huko England amedai Straika huyo ni ‘Ajali inayongoja kutokea.’
 
 Kesho Alhamisi, CAS [Court for Arbitration in Sports, Mahakama ya Usuluhisho Michezoni, itatoa uamuzi wa Rufaa ya Mchezaji huyo wa Uruguay ambae alikuwa akiichezea Liverpool na kuhamia Barcelona Mwezi uliopita kupinga Adhabu ya kufungiwa Miezi Minne kutojihusisha na kitu chochote cha Soka, Adhabu ambayo alipewa huko Brazil Mwezi Juni baada ya kumng’ata Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy.
Pamoja na Kifungo hicho, Suarez pia alifungiwa kutocheza Mechi 9 za Uruguay na kupigwa Faini Pauni 66,000.

Nae Mkuu wa FA ya England, Richard Scudamore, amesema yeye hakusikitika kumwona Suarez aikihama Liverpool kwani Mchezaji huyo ni ‘Ajali inayongoja kutokea.’
SUAREZ – Matukio yake ya utata:

-Juni 2014 – Afungiwa Miezi 4 kwa kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini
-Aprili 2013 – Afungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
-Des 2011 – Afungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Man United
-Nov 2010 – Afungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Otman Bakkal wa PSV Eindhoven

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top