Kikosi cha wapiganaji wa
kiislam wenye msimamo mkali Islamic State kimeachilia video inayoonesha
mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani aliyetekwa nyara
nchini Syria 2012.
James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria yapata miaka miwili iliyopita.Foley ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa ''Ninawaomba ndugu jamaa na marafiki wangu wasimame na kuzuia adui wangu Serikali ya Marekani kwa ukatili wanaoendelea kutekeleza ndani ya Iraq.''
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kizungu anailaumu Marekani kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
''Kila siku mnaposhambulia jamhuri ya kiislamu manadhuru maisha ya muislamu na hivyo tunachukua maisha yetu ili iwe onyo kwako (rais) Obama''
Punde baada ya kukamilisha hotuba yake bwana huyo anaanza kumchinja Foley lakini video hiyo inazimwa .
Sekunde chache baadaye mwaandishi mwengine pia raiya wa Marekani Steven Sotloff, anaonekana kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi mwa Obama na hatua atakayochukua .
Scotloff alitekwa mwaka wa 2013 nchini Syria karibu na mpaka wa Uturuki.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.
Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya mabomu yanayowalenga wa Iraq.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni