Jopo la wataalam wa shirika la
afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo
hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo
maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.
Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo
likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo
imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani
mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.Dawa hiyo ambayo haijajaribiwa imetumiwa na raia wawili wa kutoa msaada kutoka marekani ambao afya yao imeimarika,lakini kasisi huyo wa Uhispania ambaye pia aliitumia dawa hiyo ameaga dunia.
Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.
Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo.
Katika ripoti iliyotolewa leo, shirika hilo linasema “Katika hali kama hizi za kuenea kwa ugonjwa huu, na iwapo masharti Fulani yataafikiwa, jopo hili limefikia makubaliano kuwa ni jambo la kimaadili kuingilia kati kwa mijarabu ambayo haijadhibitishwa huku ufanisi wake ukiwa haujulikani na adhari mbaya, kama matibabu au kinga.”
WHO ilitangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kama janga la afya la dharura ulimwenguni.
Huku hayo yakijiri, serikari ya Liberia imesema kuwa madawa yatakayofanyiwa majaribio yatafikishwa nchini humo baadae juma hili – ingawa watengenezaji wa dawa madawa hayo Mapp Bio pharmaceutical walikuwa wameonya kuwa madawa hayo ni haba.
Zmapp imetumiwa kuwatibu wafanyikazi wawili wa US aid ambao walionyesha dalili ya kupata nafuu.
Hata hivyo, dawa hizo zimejaribiwa kwa nyani tu na bado haijatathminiwa kuwa ni salama kwa binadamu.
Shirika la afya dunini WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Africa sasa imepita watu 1000.
Hii leo wataalam hao wa WHO wamekubaliana kwamba utumizi wa dawa hizo utakubalika iwapo kutakuwa na uwazi huku rukhsa ikitolewa na wote wanaoshiriki katika tiba hiyo mbali na kuficha siri ya mgonjwa aliyetibiwa.
Na huku hayo yakijiri Liberia ambalo ndio taifa lililoathiriwa sana na ugonjwa huo lilianza kutumia dawa hizo kutoka marekani kabla ya uamuzi wa utumizi wake kutolewa na WHO.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni