KOCHA
wa Gor Mahia, Bobby Williamson ameondoka Uwanja wa Nyamirambo kwa
hasira akiwabwatukia marefa baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji
APR katika mchezo wa Kundi B Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Kagame.
“Soka ni soka, lakini huyu refa (Israel Mujuni wa Tanzania) na mshika kibendera wake wamefanya tufungwe hawafai kabisa hawa watu, mchezaji kaangushwa pale, hakupiga filimbi, mpira umeendelea kuchezwa hadi tumefungwa (bao la kusawazisha) ”alisema kwa hasira Bobby na kuondoka zake.
Gor
Mahia ilikaribia kabisa kupata ushindi wa kwanza katika michuano ya
mwaka baada ya kutoka nyuma kwa bao 1-0 kipindi cha kwanza na kuongoza
kwa 2-1 hadi sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho.
Hata hivyo, bao la dakika ya 90 na ushei la Bernabe Mubumbi akimalizia krosi ya Jean Baptiste lilizima ndoto hizo na kulazimishwa sare ya 2-2, hivyo kujiweka mguu mmoja nje kwenye michuano hii.
Jean Claude Mugiraneza alitangulia kuifungia APR dakika ya 22 kabla ya Godfrey Kizito kusawazisha dakika ya 60 na Godfrey Walusimbi kufunga la pili dakika ya 84.
Dan Sserunkuma aliifungia bao la tatu Gor dakika ya 88, baada ya kipa wa APR kuutema mpira mrefu wa kichwa wa kurudishiwa na mshambuliaji huyo akauchukua na kuutupia nyavuni, lakini refa Israel Mujuni akakataa, akisema mlinda mlango alipokonywa mpira.
Matokeo hayo yanaifanya Gor Mahia iambulie pointi ya kwanza baada ya mechi tatu na itahitaji kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya KCC ya Uganda, ili kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali kulingana na matokeo ya mwisho ya timu nyingine kwenye kundi hilo.
Katika mchezo mwingine uliotangulia wa kundi hilo, Atleitco ya Burundi imeshinda 2-1 dhidi ya Telecom ya Djibouti.
Ramadhan Niragira aliifungia Atletico bao la kwanza dakika ya 11 kabla ya Mustapha Mohamed kuisawazishia Telecom dakika ya 29 na Fiston Nzomukunda aliyetokea benchi, akawafungia bao la ushindi wawakilishi wa Burundi dakika ya 87.
APR inaongoza kundi hilo kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na KCC pointi sita, zote zimecheza mechi tatu, wakati Atletico iliyomaliza mechi zake nne ni ya tatu pointi sita, Telecom (mechi tatu) ya nne pointi tatu na Gor inashika mkia kwa pointi yake moja za mechi tatu pia.
Katika mchezo wa Kundi C, bao pekee ka Traore Mohamed kwa kichwa dakika ya 63 limetosha kuipa El Merreikh ya Sudan ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Vital'O ya Burundi, ambao sasa wanaaga michuano hiyo mapema kabisa.

bin zubiery
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni