Mwanariadha wa Ufaransa,
Mahiedine Mekhissi-Benabbad amepokonywa medali yake ya dhahabu,
aliyotarajiwa kuipata baada ya kushinda mbio za mita 3,000 za kuruka
viunzi, katika mashindano ya riadha barani Ulaya.
Kilichomkuta mwanariadha huyu kilitokana na hatua yake ya kuvua shati lake alipokuwa anaelekea kushinda mbio hizo.Awali, alionekene kupewa kadi ya manjani kama onyo na mmoja wa maafisa wa mashindano hayo ila hatimaye alipokonywa ushindi wake.
Timu ya uhispania ilionekana kuteta baada ya Murella kuvuka msitari na kuvua shati lake.
Mekhissi-Benabbad, 29, aliyeshinda medali ya fedha, siku za nyuma amewahi kusababisha utata baada ya kupigana na mwanariadha mwenza wakiwa wanakimbia mwaka 2011.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni