Hatimaye shirika la ndege la
Kenya Airways limesalimu amri na kukubali shinikizo la kusitisha safari
za ndege kuelekea mataifa matatu yaliyoathirika pakubwa na mlipuko wa
ugonjwa wa Ebola.
Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Titus
Naikuni alisema kuwa baada ya kupata ushauri wa shirikisho la Afya
duniani WHO na wizara ya afya nchini Kenya shirikisho hilo limeamua
kusimamisha safari zote za ndege kuenda Liberia na Sierra Leone.Hata hivyo shirika hilo lilisema kuwa litaendelea na safari zake kuelekea Nigeria.
Kama hatua za dharura abiria wote ambao walikuwa wamenunua tiketi za kuenda mataifa hayo watarejeshwa pesa zao .
Shirika la ndege la KQ lilikuwa limepuza shinikizo la kusafiri kuenda Magharibi mwa Afrika hatua ambayo ilikuwa imevutia wadau nchini Kenya kutishia kuishtaki mahakamani ilikuishurutisha kukomesha safari hizo kwa hofu kuwa huenda ikasababisha kuenea kwa ugonjwa huo nchini Kenya.
Shirikisho la Afya duniani WHO lilizua hofu nchini Kenya lilipoitaja kama moja ya mataifa yenye athari kubwa ya kuenezwa kwa Ebola.
Uwanja huo hupokea takriban ndege 76 kila wiki kwenda na kutoka Magharibi mwa Afrika.
Mapema juma hili athari ya ugonjwa huo wa Ebola ulipelekea shirika la ndege la Korea kusimamisha safari zake za ndege kuingia Kenya kwa hofu ya maambukizi ya Ebola.
Hadi kufikia sasa hakuna mkenya yeyote aliyepatikana na ugonjwa huo wa Ebola.
Watu zaidi ya 1000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo katika mataifa ya Sierra Leone Guinea Libera na Nigeria.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni