Wanariadha wanaotokea mataifa
yaliyoathirika na homa ya Ebola wamezuia kushiriki makala ya mwaka huu
ya mashindano ya olimpiki ya vijana yaliyoanza leo katika mji wa Nanjing
Uchina.
Kamati andalizi ya mashindano hayo iliamua
kuwatenga wanariadha watatu kutoka Guinea na Nigeria kutoshiriki
mashindano ya uogeleaji na yale yanayohusu kugusana .Kamati ya olimpiliki duniani IOC ilisema kuwa ni vigumu kuenezwa kwa homa hiyo ya Ebola japo wanachukua tahadhari hiyo kwa maslahi ya washiriki wengine.
Wanariadha wote hata hivyo watafanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Wanariadha kutoka Sierra Leone ana Liberia waliamua kutosafiri kwenda China.
Mashindano hayo yaliyoanza leo yataendelea hadi tarehe 28 Agosti.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni