Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis
Cheka ‘SMG’, amesema kamwe hawezi kufirikiria kupanda ulingoni kupigana na Mada
Maugo akibeza kuwa uwezo wake ni mdogo.
Maugo hivi karibuni alifanikiwa kumchapa
mpinzani wake, Thomas Mashali katika pambano la Usiku wa Matumaini na baada ya
hapo akatamba kwamba anamtaka Cheka.
Cheka
amesema anamshangaa Maugo kuendelea kung’ang’ania kutaka kupigana naye licha ya
kufahamu kuwa uwezo wake ni mdogo.
“Kiukweli namshangaa Maugo kuendelea kung’ang’ania
kutaka kucheza na mimi, ila atambue kuwa uwezo wake ni mdogo, haniwezi, halafu
ukiangalia rekodi zinaonyesha nilishampiga katika mapambano matatu.
“Unajua Maugo kwa kiwango chake anaweza
kucheza labda na Kalama Nyilawila lakini siyo mimi au kama anataka nimuandalie
pambano yeye aje, kwa sababu sasa
hivi nina kampuni yangu ya upromota na kesho (leo) kuna mabondia watacheza
kwenye Ukumbi wa Vijana Social Hall hapa Morogoro,” alisema Cheka.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni