Wake wa wanajeshi wa Nigeria
wameandamana Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wakipinga hatua ya jeshi
kuwatuma waume wao vitani kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kiislamu
la Boko Haram.
Maandamano hayo yaliyotokea nje ya kambi za
jeshi zilizoko katika mji wa Maiduguri ilitokea baada ya serikali
kutangaza kuwa inalenga kuukomboa mji wa Gwoza kutoka kwa wanamgambo
hao.Inakisiwa kuwa mamia ya raiya waliuawa juma lililopita wanamgambo wa Boko haram walipouteka mji huo wa Gwoza l kulingana na Seneta wa eneo hilo Ali Ndume.
Boko Haram imekuwa ikipigani kuunda jimbo linalojitawala kwa misingi ya Kiislamu kaskazini mwa Nigeria.
Kampeini ya Boko Haram ya kuwachinja wanajeshi ndiyo imewatia hofu kubwa familia ya wanajeshi hao .
Wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakilalamikia kuwa na vifaa duni na hivyo kushindwa na wapiganaji hao wa Boko Haram ambao wanatumia makombora na magari ya kisasa ya kivita .
Wanajeshi wa nigeria walimshambulia meja Generali Ahmed Mohammed, mnamo mwezi mei wakilmaumu kwa kuuawa kwa wenzao katika vita vilivyotokea katika kambi ya jeshi ya Maimalar .
Mwanamke mmoja aliyezungumza na BBC bila kusema jina lake anasema kuwa wanaume wao wamekuwa wakikabiliana na Boko Haram kwa miaka 6 sasa na kila walipouawa hakuna msaada waliopata kutoka kwa jeshi.
''sasa hii leo wanataka kutuma waume wetu huko Gwoza ?
''Hatutakubali hilo kamwe !''
Wakaazi wa mji huo uliotekwa na kundi hilo wanasema kuwa miili ya watu ingali imetapakaa ovyo mabarabarani ikioza zaidi ya juma moja tangu Gwoza itwaliwe na kundi hilo.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni