MABINGWA na wawakilishi wa Tanzania Bara, Azam fc
wametupwa nje ya michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na kati,
Kombe la Kagame kwa kufungwa penalty 4-3 dhidi ya El Merreik ya Sudan
katika mchezo wa robo fainali.
Mshindi wa mchezo huo uliopigwa
katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda, alilazimika kupatikana kwa
changamoto ya matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana
(0-0).
Mechi hiyo ilikuwa ngumu kwa timu
zote kwani mashambulizi ya kupangwa yalitawala kwa pande zote.
Azam walikosa nafasi kadhaa za
kufunga kupitia kwa washambulaiji wake,Kipre Herman Tchetche, John Bocco na
Leonel Saint-Prexu, lakini nao Merreikh ambao wana historia kubwa katika soka
la ukanda huu walishindwa kuzitumia vizuri nafasi walizopata.
Hata hivyo huwezi kuacha kumsifu
kipa wa Azam fc, Mwadini Ali kwasabbau aliokoa michomo ya hatari langoni mwake
ambayo ilikaribia kuingia nyavuni.
Penati tatu za Azam fc zilifungwa na
beki wa kati Aggrey Morris, mshambuliaji alitokea benchi, Mrundi, Didier
Kavumbagu na Erasto Edward Nyoni.
Beki wa kulia Shomari Salum Kapombe
na Mshambulaiji, Mhaiti, Leonel Saint- Prexu alikosa penalti yake.
Kwa matokeo haya, Azam fc kesho
wanasafiri kurudi Dar es salaam Tanzania,wakati Merreikh wanamsubiri mshindi wa
mechi ya pili inayoendelea muda huu baina ya KCC ya Uganda na Altabara ya Sudan
kusini.
Nusu fainali moja imeshajulikana
ambapo timu mbili za Rwanda, Polisi na APR zitachuana baada ya kushinda kwa
penalti pia katika michezo ya jana.
Polisi waliifunga Atletico kwa
penati 9 kwa 8, wakati APR waliitoka Rayon Sport kwa penalti 4 kwa 3.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni