LOGO

Italy imemteua aliekuwa Kocha Mkuu wa Juventus Antonio Conte kuwa Kocha wa Timu ya Taifa yao hadi Mwaka 2016.
Cheer up,  Antonio! Conte will be appointed the manager of the Italian national team after the 2014 World Cup
Conte anarithi wadhifa huo kutoka kwa Cesare Prandelli ambae alijiuzulu mara baada ya Italy kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni huko Brazil waliposhindwa kuvuka hata hatua za Makundi.
Conte, mwenye Miaka 45 na Kiungo wa zamani wa clabu ya Juventus na Italy, alijiuzulu ghafla Juventus, ambako kwa Misimu Mitatu iliyopita aliipa Ubingwa mara tatu mfululizo, mara tu baada ya kujiuzulu kwa Prandelli lakini wakati huo haikusemwa chochote kwanini alifanya hivyo.
 Energetic: Conte is expected to be officially revealed as the Italy manager on Friday at the latest
Mbali ya kuwa Kocha Mkuu wa Juve, Conte pia aliwahi kuziongoza Klabu za Bari na Siena na kuzipandisha kutoka Ligi Serie B kwenda Serie A na pia alifanya kazi na Klabu za Arezzo na Atalanta.
Wakitangaza uteuzi wa Conte, Shirikisho la Soka la Italy limesema Kocha huyo, mbali ya Mshahara wake, atapata Bonasi ikiwa Italy itafuzu kucheza Fainali za EURO 2016 na pia Bonasi nyingine wakipanda Nafasi 5 kwenye Listi ya Ubora ya FIFA ambayo sasa wako Nafasi ya 5 na Bonasi ya Tatu ikiwa watatinga Fainali halisi ya EURO 2016.

BORN: Lecce, Italy, July 31 1969 (age 45)
2006-2007: Arezzo
2007-2009: Bari
2009-2010: Atalanta
2010-2011: Siena
2011-2014: Juventus 

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top